Balozi wa kudumu wa African Union Mhe. Amina Salum Ali (pichani) akihutubia katika mkutano wa Africana conference ' unaofanywa kila mwaka na TUFTS University (Fletcher college) .Hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo uliobeba ujumbe wa 'Africa in the global Arena'.Balozi Amina S alum Ali alikuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huu tarehe 20 mwezi wa Februari 2015 huko Boston Massachussets.
katika hotuba yake alichukua nafasi kuzungumzia masuala ya Afrika na umuhimu wa bara la Afrika kuwa mhimili mkuu katika shughuli za maendeleo ya Dunia .Pia alielezea juu ya sera za maendelo za Umoja wa Afrika za mlengo wa miaka 50 kwa kifupi Agenda 2063 zinazolenga kufanya mageuzi makubwa kwa bara la Afrika katika nyanja za uchumi ,siasa ,maendeleo ya jamii ,utamaduni na maeneo yote yanayowagusa wananchi wa Afrika
Agenda 2063 ni maamuzi ya kuzitaka serikali za Afrika kuchukua hatua za utekelezaji ambazo zitabadili mwenendo wa sera za uchumi na manedeleo ya jamii kwa kuleta ufanisi wa haraka wa maendeleo ya Afrika ambayo wenyewe wa Afrika wameya pendekeza yafanywe katika miongo hii ya miaka 50 hadi mwaka 2063.
kwa kufuatilia maendeleo ya bara la Afrika katika miongo ya miaka 10 iliopita Afrika kwa kufuatilia sera sahihi za kusimamia uchumi na kuweka vipaumbele vitakavyo shajiisha ukuaji wa uchumi na zitakazoweza kusaidiana katika ukuaji wa kisekta na hasa kwa kutumia rasilmali zetu .kuna uwezekano mkubwa kuwa karne hii ikawa karne ya Afrika na pia kuweza kuwa mhusika katika masuala yanayo endesha dunia kwenye maeneo ya Uchumi , na siasa.
No comments:
Post a Comment