Balozi mpya wa Senegal nchini Marekani Mhe, Babacar Diagne alipotembelea ubalozi wetu mapema leo hii Jumanne tarehe 10/02/2015.
Mhe, Babacar Diagne akikaribishwa na mwenyeji wake Mhe, Liberata Mulamula kwenye Ubalozi wa Tanzania Washington, DC.
Mabalozi hao wawili wakibadilishana machache kuhusu mambo yanayokabili bara la Africa kwa ujumla pamoja na uwepo wao kama mabalozi nchini Marekani.
Mabalozi hao wawili pichani wakiwa na mmoja wa maafisa wa Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani Dr, Switbert Mkama
Mhe, Babacar Diagne balozi wa Senegal nchini Marekani akiwa na wenyeji wake Mhe, Liberata Mulamula na Afisa wa Ubalozi Dr, Switbert Mkama pamoja na afisa aliyeambatana naye leo hii .
PICHA ZOTE KWA HISANI YA CAMERA YA UBALOZI.
1 comment:
nawapenda wasenegales wako kama wamasai wetu kwa urefu wao na roho zao nzuri.wengi wao wakike na wakiume ni warefu na tena ni wazuri ila sipendi tabia zao wote wakike na wakiume ni wajeuri na wajuaji nimeisha kwao sana na nasema kikabila chao na ni wakarimu, sema sipendi hiyo tabia yao zao zao za kibabe babe na kijeuri jeuri na ujuaji.
ni vizuri kuwa na uhusiano nao.
Post a Comment