Wapendwa wasomaji, wiki iliyopita
niliwaletea mahojiano maalum kutoka kwa dada Zawadi Kakoschke. Katika
mahojiahano hayo moja ya maswali ambayo nili muuliza ni kama kuna
huusiano kati ya majina ambayo wazazi wanawapa watoto wao na mafanikio
au tabia ya watoto hao. Sehemu ya mahojiano hayo yalikuwa kama
ifuatavyo:-
Wewe binasfi unaamini majina
ambayo wazazi wana wapa watoto wao yanachangia katika mafanikio yao
kiuchumi, kielimu, na tabia zingine? Kwa mfano majina kama Amani anaweza
akawa mtu wa kupenda amani siku zote, au majina kama Tabu, Sikujua
yanaweza yaka changia mototo kuwa na matatizo katika maisha yake?
Majina yanachangia sana katika maisha ya watoto wetu. Ndio maana mimi
nilijitahidi sana kukaa na kufikiria majina ya kuwapa watoto wangu.
Nimekua naamini hili kwa miaka mingi sana kuwa majina yana nguvu sana
katika kujenga au kubomoa maisha ya muhusika. Huwa nashukuru sana kwa
wazazi wangu kuamua kunipa jina la Zawadi nina imani kubwa hili jina
limenisaidia kwa namna moja ua nyingine.
Kwakweli majibu ya dada Zawadi
yalinikumbusha binamu yangu mmoja aitwaye Tabu Obago. Nakumuomba nifanye
mahojiano naye mafupi haswa kutaka kujua kama jina lake limekuwa nuru
kwakwe au la! Na hivi ndivyo ilivyo……
Kusoma zaidi mahojiano haya ponyeza HAPA

No comments:
Post a Comment