Baadhi ya Sehemu za jengo la Jiko la Hoteli ya Kendwa Rocks iliyoko Mkoa wa Kaskazini Unguja ambalo iliuungua moto ulisababishwa na hitilafu za umeme.
Wahandisi wa Hoteli ya Kendwa wakijaribu kurejesha miundo mbinu ya umeme iliyoathirika kutokana na moto mkubwa uliotokea kwenye Hoteli hiyo.
Jengo la Jiko la Hoteli ya Kendwa Rocks lililoungua vibaya mwa moto uliosababishwa na hitilafu ya umeme.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji Mwakilishi wa Hoteli ya Gold Zanzibar iliyopo Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja Bwana Andrea Azzala baada ya paa la jengo lao kuungua moto.
Balozi Seif akikaguzwa kuangalia maeneo yaliathirikia kutokana na moto kwenye Hoteli ya Kendwa Rocks Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kulia ya Balozi Seif ni Msaidizi Menja Mkuu wa Kendwa Rocks Bwana Omar Ibrahim Kilupi, Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassim Tindwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d.
Balozi Seif akiwafariji wamiliki wa Kendwa Rocks Bwana Ali Ibrahim Kilupi aliyepo mwnzo kushto na msaidizi wake Omar Ibrahim Kilupi baada ya jengo la jiko la hoteli yao kuungua moto.Kati kati ni Waziuri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na kushoto kwa Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Kaskazini Unguja Kanal Mstaafu Juma Kassin Tindwa.
Picha na – OMPR – ZNZ.
No comments:
Post a Comment