Alisema Cheka alijichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mtu na mahakama haitazami mtu maarufu au kuangalia sura ya mtu zaidi ya kufuata sheria na kutoa hukumu.
MKUU wa Mkoa wa Manyara, Dk Joel Bendera, amesema bondia Francis Cheka amefanya uzembe hivyo kuhukumiwa kwenda gerezani ni haki yake na fundisho kwa wasanii na wanamichezo wanaojichukulia sheria mkononi.
Dk Bendera ambaye mwaka 1980 aliweka rekodi ambayo haijavunjwa ya kuwa kocha wa Taifa Stars iliyofuzu mashindano ya Kombe la Mataifa Huru ya Afrika (Afcon) nchini Nigeria, aliyasema hayo juzi Jumamosi mjini Babati kwenye Siku ya Sheria.
Alisema Cheka alijichukulia sheria mkononi kwa kumpiga mtu na mahakama haitazami mtu maarufu au kuangalia sura ya mtu zaidi ya kufuata sheria na kutoa hukumu.
“Nilipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Cheka alipochukua ubingwa wa Dunia tulimfanyia sherehe kubwa tukampatia kiwanja na vitu vingi tu vizuri kwa lengo la kumuenzi, lakini amevunja sheria na sasa amefungwa,” alisema Dk Bendera. Alisema kuna watu walimpigia simu kuwa Cheka amefungwa hivyo awasaidie wamtoe ilhali ameshahukumiwa kwenda jela miaka mitatu jambo ambalo haliwezekani tena kwani mahakama imetimiza wajibu wake.
Alisema kila mhimili unajitegemea na haiwezi kuingiliana, hivyo Serikali ina wajibu wake, mahakama nayo ipo kwa namna yake na Bunge lipo peke yake, kwa hiyo kila mhimili unatimiza kanuni, taratibu na sheria za nchi.
Source:Mwanaspoti
3 comments:
that's all about the rule of law, haina mtu maarufu wala mtu muhimu. ukizingatia zaidi kupiga watu kwa sababu unajua kupigana, na aende jela ndio atajifunza kuheshimu watu.
what about Chenge?
kama chenge atapiga watu naye ashtakiwe vile vile, and what about you anonymous of 5:43
Post a Comment