Advertisements

Friday, February 27, 2015

NDANI YA MASAA 24: ISMAIL JUSSA ATA-UNGURUMA WASHINGTON D.C., FEB 28, 2015


Ismail Jussa (Muwakilishi wa Stone, Town, Zanzibar) kupitia chama cha CUF na mjumbe wa UKAWA atakuwepo Washington, D.C. (DMV) kuongea na waTanzania Jumamosi February 28, 2015 kuanzia saa 10 jioni hadi mbili usiku (4pm-8pm). Zingatia muda

Agenda;
Mchakato wote wa Katiba mpya
Ufafanuzi juu ya muundo wa serikali tatu
Uamuzi wa UKAWA kususia mchakato huo dhalimu 
Kwa nini Diaspora walitengwa kutoa maoni na uraia pacha
Maswali na majibu bila kikomo


Address: TABEER HALL 
1401 UNIVERSITY BLVD, HYATTSVILLE, MD

7 comments:

Anonymous said...

Tunakuja kusikiliza katiba ya wananchi

Anonymous said...

sasa mbona katika agenda tayari mmeanza na propaganda kwamba mchakato dhalimu!!!! sasa hizi lugha mbona za jazba,kweli huu mkutano utakuwa na manufaa kama waandaji wenyewe wanaanza kutumia maneno kuwapa ukweli diaspora, mchakato dhalimu!!!! mwanadiaspora gani ambaye hajui mchakato mzima kabisa wa katiba yetu, bwana jussa yeye mwenyewe alisusia mchakato pamoja ukawa wakatoka nje lakini bado wakawa wanachukua posho za vikao!!! sasa kama anawakilisha wananchi halafu anatoka katika vikao wala hahudhurii na kuchukua posho naona hapo kuna walakini!? njia ya kutatua tatizo sio kukimbia ni kulikabili, sasa huo ukweli anataka kutuambia ni upi wakati hata vikao hakuhudhuria??!! tafadhali angalieni lugha mnazotumia, inasound kama vile ni kivyama vyama badala utanzania. luka ni kuelimisha tu usiibanie mpwa.

Anonymous said...

Kwanini diaspora walitengwa kutoa maoni ya ya uraia pacha? Si tulikuwa na Mwakilishi. Let's not exaggerate issues even if we have differences!!

Anonymous said...

Huyu mwarabu anataka kutuambia nini haki za wabongo???Kama anazijua sana atujibu kwanini babu zake waliuza watumwa?

Anonymous said...

kama humjui jussa kabila gani basi kaaa kimya wewe,utafanya la maana sana ukiwa hivyo la si hivyo utakuwa bonge la mbururaaa,bata mzinga kuogelea hawezi kazi kuchezea majitu ndo unachokifanya.

yani jussa muarabu na wewe ni nani?

na wewe kwa nini unawashujudia wazungu walio kuuzia babu zako?

wewe humpati jussa hata chembe ya mtama kwa usomi alionao na experience za nchii hii.

next time kuwa mstaarabu kama huna la kusema kaa kimya usijitia ujuaji kumbe mbururaaa mkubwa.

unachangia tu ili uonekana wakati unajishusha na kuandika pumba.

jiheshimu utaheshimika vicha udhaifu wako kama hujui kitu au watu utaheshimika.ukiwa mropo mropo utaropotekaaaa.

dj luke please usibaniye comment hii please.

Anonymous said...

Mkuu luca na vijimambo team tafadhalini waungwana mnaweza kutuwekea ka clip cha huu mkutano sema hivi kwa niamba ya wengine tuliopo state za mbali na tutoweza kuhudhuria huko Washington.
Tufikiriyeni tafadhalini.

Anonymous said...

maswali na majibu bila ya kikomo,safi sana hivi ndo inavyotakiwa na hivi ndo kukuwa kwa mwana siasa msomi.si kuzuiya watu wasiulize na kukaa kumsikiliza mheshimiwa na kumpigia makofi na kila akisemacho ndio baba ndio baba.wakati huo kwa kizazi cha kuona mbali hakuna tija.

karibu sana jussa Washington dc