Binti wa jumuiya ya Dawood Bohra nchini Tanzania, akiwa ameshikilia bango lenye picha ya Sheikh Syedna Burhanuddin (RA), wakati wa kuadhimisha siku ya kuzaliwa kiongozi wa 53 wa madhehebu hayo, Syedna Mufaddal Saifuddin, (TUS), jijini Dar es Salaam Jumamosi jioni, Februari 14, 2015. Maadhimisho hayo yalipambwa na matembezi ya waumini wa madhehebu hayo, ambapo vijana walionyesha vipaji vyao, michezo namavazi mbalimbali yakiwemo yale ya kimasai. Pia matembezi hayo yaliongozwa na brass band ya jeshi la magereza. Mwakilishi wa kiongozi huyo hapa nchini, Sheikh Tayabali Sheik Hamza, alikata keki kuashiria siku ya kuzaliwa kwa kiongozi huyo anayeheshimika sana Duniani
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog












No comments:
Post a Comment