Bobby Brown akiwa nje ya hospitali ya chuo kikuu cha Emory siku ya Alhamisi Feb 5, 2015 kwenye siku yake ya kuzaliwa akipokua ametoka kwa ajili ya kuvuta sigara.
Bobby Brown akiongozana na familia ya Houston alipokua akiwasili hospitali mapema leo Alhamisi kumjulia hali mwanae Bobbi Kristina ambaye yupo kwenye koma. Familia ya Houston imekuwanae sambamba tangia siku ya kwanza ya maswahibu ya mtoto Bobbi Kristina.
Bobby Brown akiongozana na Gary Houston ambaye ni mpwa wake Whitney Houston.(Picha zote kwa hisani ya Ok Magazine)
Madaktari wameiambia familia ya Bobbi Kristina kwamba kwa sasa hakuna wanachoweza kufanya kuokoa maisha ya mtoto huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye Jumamosi iliyopita alikutwa amelala kifudifudi bafuni nyumbani kwake na baadae kudunduliwa na mchumba wake Nick Gordon akiwa na marafiki zake na kutoa taarifa polisi na Bobbi Kristina kuwahishwa hospitali ambako alikutwa ubongo kuishiwa na hewa ya oksijeni iliyopelekea ubongo wake kushindwa kufanyakazi na kuwa kwenye koma tangia siku hiyo.
Chanzo cha karibu na familia kimesema uamuzi wa kuondoa mashine upo mikononi mwa baba yake ambaye ameomba apewe muda mpaka Jumamosi hii. Leo Ijumaa Februari 5 ni siku ya kuzaliwa ya Bobby Brown na yeye anaamini kwamba Bobbi Kristina anaweza kuzinduka kwani mmoja ya wanafamilia alishazinduka siku za huko nyuma alipokaa kwenye koma kwa siku 8.
Bobbi Kristina alihamishiwa hospitali ya chuo kikuu cha Emory siku ya Jumanne Februari 3, 2015 ambayo imeelezewa kuwa na huduma bora zaidi. Kifo cha Whitney Houston kilitokea baada nae kukutwa ameanguka bafuni na kichwa chake kikiwa kimeinamia chini kama alivyokutwa Bobbi Kristina.
No comments:
Post a Comment