Zawadi Kakoschke |
Naomba utueleze Historia yako kwa ufupi: Naitwa
Zawadi Owitti Kakoschke, mama wa watoto wawili Amani na Malaika na mke
wa Bart Kakoschke. Nimezaliwa miaka 39 iliyopita huko Songea, Tanzania.
Ni mtoto wa pili wa marehemu Fatuma ambae anatokea mkoani Iringa. Mimi
ni mjaluo baba yangu anatokea Shirati Rorya mkoani Mara. Kwa sasa makazi
yangu yako kwenye nchi za kiarabu ambapo mume wangu anafanyia kazi.
Wewe ni mmiliki wa blog ya
maisafari.com, ambayo hata mimi ni shabiki mkubwa sana wa blog yako. Je
nini haswa kilipelekea wewe kuanzisha blog yako? Nilitaka
kuhamasisha watanzania wenzangu kupenda mambo ya utalii na kwa kiasi
kikubwa nimefanikiwa kwa hilo. Nitatoa mfano nchi yetu ya Tanzania ina
vivutio vingi sana lakini sababu hatuna utamaduni wa kupenda utalii watu
wengi hawajaribu hata kwenda kuangalia ni kitu gani haswa kinawafanya
watu watoke nchi mbali mbali kuja kutembelea nchi yetu. Mimi kama
mtanzania ambae napenda sana mambo ya utalii nikaona kuna haja ya
kuwahamasisha watanzania wenzangu kwa njia ya blog ambapo huwa naweka
picha na maelezo mbali mbali ya nchi ambazo nimefanikiwa kutembelea.
kuendelea kusoma mahojiano haya ponyeza HAPA
No comments:
Post a Comment