Hata hivyo, amsema serikali inaangalia ripoti ya Swiss Leaks ili kuona uhalali wa akaunti hizo za siri.
“Sisi hatujaona kama ni kosa kwa Watanzania kuwekeza fedha zao kwenye mabenki ya nje na wala isionekane kama ni jambo haramu kabisa.
Kama serikali tungetamani wawekeze kwenye benki nchini ili kukuza sekta ya fedha lakini pia hatuwafungi kutowekeza nje,” alisema.
“Tunachofanya ni kuiangalia hiyo ripoti ili kujua ukweli wa taarifa hizo, lakini taarifa hiyo haimaanishi kwamba ni kosa kubwa kisheria kwa Mtanzania kuweka fedha nje,” alisema.
Mkuya alisisitiza kuwa hakuna shida yoyote kwa Watanzania kuweka fedha kwenye akaunti nje ya nchi.
Waziri Mkuya ameyasema hayo siku moja tu baada ya vyombo vya habari nchini kuripoti taarifa ya kuwapo vigogo 99 wa Tanzania kuficha mabilioni ya shilingi katika benki za Uswisi kutokana na ripoti ya mtandao wa Swiss Leaks chini ya Waandishi wa Habari za Uchunguzi wa Kimataifa (ICIJ).
Taarifa ya Swiss Leaks iliyotolewa juzi Jumapili, inaonyesha kuwa vigogo hao wa Tanzania wana akaunti za siri zenye Dola za Marekani milioni 114 ambazo ni sawa na Sh. bilioni 199.6.
Msingi wa ripoti hiyo umetokana na aliyekuwa mfanyakazi wa benki ya kimataifa HSBC, Hervé Falciani, kuvujisha siri za akaunti za wateja baada ya kuacha kazi; na mwaka 2008, alivujisha siri za akaunti za siri za baadhi ya watumishi wa umma na wanasiasa kwa Serikali ya Ufaransa ambayo mamlaka za kodi nchini humo ilifanya uchunguzi na kuthibitisha.
Ripoti hiyo ya Swiss Leaks, inaeleza kuwa taarifa za kiuchunguzi kutoka benki ya HSBC nchini Uswisi zinaonyesha kuwa akaunti hizo zinahusishwa na baadhi ya wanasiasa, wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa umma ambao wamejipatia utajiri wa siri unaotokana na kampuni hewa (offshore companies).

CHANZO: NIPASHE
3 comments:
Kama sio kosa serikali ilikosea kuruhusu watu kuweka pesa nje ya Tanzania. Wewe huna imani na Tanzania wala huna hisia na watanzania. Itakuwaje pesa zimepatikana nchini eti watu wa nchi nyengine wakanufaike. Wewe hujui kwamba kwa mtindo huu wa kupeleka fedha ndio pesa zetu zinashuka thamani, vitu vinapanda bei na kuzidisha umaskini. Fedha hii ilioko nje ya nchi haipati kuzunguka nchini na kwa hivyo uchumi unakua duni. Wewe upo hapo kwa masilahi ya nchi na wananchi. Ndio nyinyi mnao idhalilisha foreign exchange yetu. Kwa statement yako ningekua Rais wa nchi ningekwambia uwachie ngazi ujiuzulu au ningekufukuza kazi. Inaonyesha hujakomaa kiuchumi na kisiasa.
wewe anonymous wa 12:53 wacha siasa zako za kijinga hapa huwezi kumuamulia mtu wapi aweke pesa zake eti ungekuwa rais ungemfukuza kazi ndio maana hukuwa rais kwa roho yako mbaya. acha mambo ya kidikteta ya kipumbavu katafute pesa zako halafu utaamua kuziweka huko unapotaka
Wewe anonymous @ 2:22 am. Sikujua kwamba wako wengi wasiopendelea nchi yetu iendelee. Ndio maana mabilioni yanaibiwa, jasho la wananchi, akina Escrow. Hata wewe kumbe ni nyangau? Tutaendelea kuomba omba mpaka lini. Nchi hujengwa na wananchi lakini wengine wanabomoa.
Post a Comment