Muswada wa Sheria ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara hautajadiliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma baada ya serikali kuuondoa kwa maandalizi zaidi.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisema jana usiku kuwa wameamua kuuondoa muswada huo ili kupata fursa ya kutoa elimu zaidi kwa viongozi wa dini na kuufanyia marekebisho baadhi ya maeneo.
Alisema serikali inatarajia kuurejesha tena bungeni mwezi ujao. Hata hivyo, habari za uhakika kutoka Dodoma zinasema kuwa kulikuwa na mvutano mkali ndani ya kamati ya Bunge iliyokuwa inashughulikia muswada huo uliokuwa kwa misingi ya imani hivyo busara ilitumika kuahirishwa uwasilishwaji kwa mara ya pili kwani mjadala kwenye Bunge zima ungeweza kuleta mpasuko.
Muswada huo ulikuwa unawasilishwa kutokana na ahadi ya serikali kwenye Bunge Maalum la Katiba ambako mjadala ulikuwa mzito baadhi ya wajumbe wakitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba Inayopendekezwa, lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akashauri kutungwa kwa sheria ya mahakama hiyo, badala ya kuuingiza kwenye katiba.
Tangu serikali itangaze kuwa itawasilisha muswada huo bungeni, kumekuwa na mvutano ndani ya jamii, kundi moja likiupinga kwa madai kuwa serikali haipaswi kujihusisha na masuala ya dini kama katiba inavyoelekeza. Ilielezwa kwamba kama Waislamu wanahitaji mahakama hiyo, basi waunde kwa njia zao wenyewe bila kuhusisha serikali.
Hata hivyo, serikali ilisema kuwa imeandaa muswada huo ili kuweka utaratibu wa kuundwa kwa mahakama hizo kisheria, lakini suala la uendeshaji wake na gharama hazitabebwa na serikali bali Waislamu wenyewe.
Tayari jumuiya za Kikristo kupitia maaskofu wao wamekwisha kutoa msimamo wao juu ya mahakama hizo wakisema kuwa siyo jukumu la serikali kuzianzisha.
SOURCE:UDAKUSPECIAL

4 comments:
Hili jambo la kadhi halikuanza aleo wala jana tangu Mheshimiwa Augustine Mrema aliweke wazi na likaendelea kupigwa chenga kuna jambo na sidhani kama litakaa liwepo!!Kazi kwa waislamu na haki!!
Haki gani kwa waislamu? Tanzania ni nchi ya kidemocrasia!! narudia tena ni nchi ya kidemocrasia!!! hivi hawa viongozi wetu naona wamechoka na uwepo wa amani tanzania, nchi gani ya democrasia ndani yake kunakuwa na sheria nyingine ambayo itakuwa inapinga ule udemocrasia? mfano mdogo ulikwishatokea kwenye sensa, kuna waislamu walisema wao hawawezi kuhesabiwa wakapelekwa mahakamani sijui imekwishaje, sasa tunaambiwa watajitegemea kwenye mahakama yao, wakati hoa hao ni walipa kodi, baada ya muda watasema tunataka kodi zetu ziendeshe shughuli zetu, hiyo yote ni ndani ya tanzania, mtagawaje hizo kodi, pia basi kuwepo na usawa kuwepo na mahakama ya kikristo ambayo kwa tanzania ndio dini mbili kubwa!!!! viongozi tumieni busara zenu acheni ujinga kukimbilia kila kitu bungeni, ni hayo tu mkereketwa
Nchi yetu ,au serikali yetu haina dini,ila watanzania wana dini zao,kama hili limepita ,miaka ijayo milango ya mambo kama haya ,imefunguliwa,serikali yetu muda ukifika ,ondoa mambo ya kisiasa ,na kuweka uzalendo mbele,tutakuwa na gharama kubwa sana,kwa sababu mahakama kuu,au mahakama za mikoa na wilaya,zitakuja kuwa na miingiliano katika maamuzi,huwezi kuwa na serikali mbili,au viongozi wawili wenye vyeo sawa katika idara moja ,iliyo fanana,hekima inatakiwa sana katika maswala haya ya maamuzi,Mungu tusaidie,kiu hii,itaanzisha safari nyingine,na nyingine,na nyingine.
Anonymous 2
kuwepo kwa mahakama ya kikristo sio tatizo mdai tuu na nyie.
kwa sababu waislam wana sharia zao za ndoa, talaka, mirathi,malezi ya watoto n.k.
mambo haya mahakama ya kawaida hawawezi kushughulikia mpaka kuwepo na chombo maalum cha waislam washughulikie wenyewe kwa sababu wanaendana na quran.
sasa kama wakristo na wao wana sharia zao kama waislam walivyokuwa nazo basi na wao wadai mahakama yao sio tatizo.
possibility wakristo hawana ndio maana wanaona hakuna haja ya waislam na wao kutumia sharia zao.
Post a Comment