Nyakaho Marungu akiwa kwenye pozi na rafiki yake Fauzia ambae wote wamemaliza kidato cha nne Baobab Secondary School.
Mama mzazi wa Nyakaho, Celestina Maro (kushoto)
MSICHANA Nyakaho Marungu (16) mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Baobab,iliyopo Mapinga Bagamoyo mkoani Pwani aliyeibuka mwanafunzi bora wa mtihani wa kidato cha nne mwaka 2014 nchini, amewataka viongozi nchini kuwa wakweli na waadilifu ili kuiletea nchi maendeleo na kutokumuudhi Mwenyezi Mungu.
Akizungumza na GPL nyumbani kwao Kitunda, jijini Dar es Salaam, amesema wanafunzi wanaofanya vizuri wako wengi, ila hawapatiwi nafasi ya kuendelezwa taaluma zao. Aidha msichana huyo ametoa ushauri kwa wanafunzi kutenga muda wa kusoma kwa bidii na muda wa kupumzika huku wakimtegemea Mungu.
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)
No comments:
Post a Comment