ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, February 18, 2015

MWANAMUZIKI CHID BENZ AKIRI MASHITAKA YAKE MATATU MAHAKAMANI LEO

Rashidi Makwiro (29), maarufu kama Chid Benz akiwa eneo la mahakama. (Picha na Maktaba yetu)

MSANII wa Muziki wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva), Rashidi Makwiro (29), maarufu kama Chid Benz leo amekiri mahakamani mashitaka matatu yanayomkabili ya kukutwa na Dawa za kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.
Chid Benz alikiri mashitaka hayo baada ya kusomewa upya hati yake ya mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema.

Hakimu Lema alisema kwa kuwa mshtakiwa amekiri mashitaka yake mahakama yake itasikiliza maelezo ya awali Februari 23, mwaka huu.

Kabla ya kutolewa amri hiyo, Wakili wa Serikali, Diana Lukondo, aliomba kumsomea mshtakiwa mashitaka yake upya.

Hakimu aliridhia ombi hilo.

Lukondo alidai kuwa Oktoba 24, mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikutwa na dawa za kulevya aina ya heroin isivyo halali zenye uzito wa gramu 0.85.

Ilidaiwa kuwa katika shitaka la pili, siku na eneo la tukio la kwanza, mshtakiwa alikutwa na gramu 1.72 za bangi isivyo halali.

Wakili huyo wa serikali alidai kuwa, siku na eneo la tukio la kwanza na la pili, mshtakiwa alikutwa akiwa na vifaa vinavyotumika kuvua dawa za kulevya aina ya heroin, kigae na kijiko huku akijua ni kosa.

Chid Benz alikiri mashitaka yote matatu, atasomewa maelezo ya awali Jumatatu ijayo na dhamana yake inaendelea.
:CREDIT:GPL

2 comments:

Anonymous said...

si alimpiga dada wa watu ray c huyu na kukana kwamba hatumi mambo haya.sasa kipo wapi bado yule mnyama mnyama naye siku zake zina hesabiwa.

jamaa kakonda kukaa ndani mchezo.

but all is all maskini tumuombe mungu amsaidiye na mungu amlani na kuwalani wanaotajirika kupitia mingongoni mwa vijana wetu,na kufanywa mapunda wakubeba mivigo hii wakati wao wamejituiza tuli majumbani mwao na maofisini mwao.

laana ya mungu iwe juu yao daima amen.

Anonymous said...

si alimpiga mdada ray c alivyomuambia achee kutumia madawa sasa niaje alivyombishia hatumii.

na bado yule mnyama mnyama.

Rashid chez benz ni kidaga kidogo sana kuna manyangumi wakubwa sana wanajulikana mbona hawakamatwi.

mkuu ana listi yao mbona hawajakamatwa mpaka hii leo? niaje hapo.

mwenye akili atajiuliza sana.

mungu awalani wanao wafanya vijana wetu kuwa mapunda wa kubeba mizigo yao hii.


maskini tumuombea sana,mtizame alivyokonda cheza kukaa ndani wewe.