ANGALIA LIVE NEWS

Friday, February 13, 2015

MWIZI AKAMATWA CHUO KIKUU MZUMBE ANUSURIKA KIFO NA WANAFUNZI WENYE HASIRA KAL

chumba kilichopo sammit hostel ya mkwawa ambacho mwizi huyo alipokuwa amefungiwa kwa nje mara baada ya kuingia ndani kwa kutumia funguo malaya ikisadikiwa kuwa anataka kuiba laptop.
Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema kuwa wanafunzi wa chuo kikuu mzumbe jioni hii wanusurika kumuua mwanafunzi mwenzao ambae anasoma mwaka wa pili chuoni hapo kwa kufanya jaribio la kuiba katika chumba namba 403 kilichopo gorofani sammit katika hosteli ya Mkwawa kwa kufungua mlango kwa funguo malaya ambapo inasemekana kumbe ndani kulikuwa na mtu na ndipo alipoingia ndani na kuwekwa chini ya ulinzi na kufungiwa kwa nje, uongozi wa chuo kwa 
polisi wakifanya jitihada za kumshusha mwizi kutoka gorofani alipokuwa akiiba
mwizi kishushwa chini ya hostel ya mkwawa akiwa chini ya ulinzi mkali wa askali polisi
mwizi akiingizwa kwenye gari la chuo tayari kupelekwa kituoni
wanafunzi wakiwa na jazba kubwa ya kutaka kumuua mwizi huyo anayesoma mwaka wa pili chuoni hapo
kushirikiana na mama dean wa chuoni hapo na uongozi wa serikali ya wanafunzi ndipo ulipoamua kuita polisi na kufanikiwa kumtoa kwa utata kwa kuwa wanafunzi walikuwa na hasira kali ya kutaka kumuua.

Chuo kikuu mzumbe ni chuo kimojawapo Tanzania ambacho kinakabiliwa na tatizo la wizi wa Laptop ambapo inasemekana kwa kipindi hiki cha mitihani kwa week huibiwa wastani wa laptop tano ambapo inadaiwa hata leo hii siku ya tukio imeibiwa laptop moja huku mwenyewe mali akiwa katika chumba cha mtihani.

1 comment:

Anonymous said...

wanaanza huko huko vyuonii wakitoka na madegree yao na ma phd yao wanakuwa wezi waliokubuhu halafu wanawasanif wenzao eti hawakusoma kumbe wao wanakwenda kusomea wizi.kikulacho kingo kuoni mwako tizama amefika stage ya kutengeneza ufunguo bandia na kuingia ndani ya chumba unadhani huyu hana ukaribu na huyo aliyetaka kumuibia anazuga zuga wanasoma pamoja kaona ufunguo wa jamaa akauchukua na kuukopi halafu anakuja kumuibia kiulani.

wanaanzaka huko huko mavyuoni uwizi wao na wakipata vyeo wanaendeleza wizi wao kwenda mbele kwa mbele. hata akiwa mkuu wa aina yeyote yeye kazi kukomba mali na wizi kwenda mbele kwa mbele.

siku za mwizi arbaini so hiyo ndo arbaini yake.