Advertisements

Thursday, February 5, 2015

NGOMA, NGOMA, NGOMA OYEEEE…

Kitoto ni ngoma ya Kusini, Tanzania. Kitoto kwangu ni mashangilizi ya ngoma na utamaduni wa Mwafrika.
Hizi ni baadhi ya shughuli ambazo mwana Kitoto hufanya ughaibuni. Usiku na mchana. Ninazionea fahari…
Miaka mingi wengi wameniuliza watakujaje Majuu. Njia nzuri na rahisi sana ni kufanya mambo ya kwetu. Ngoma ni kitu kinachopendwa na wageni maana ni uhalisia na asili ya Mwafrika.
Juu hapa wanaonekana wanamuziki wawili wa Kitanzania wanaoishi Uingereza. Saidi Kanda na Fab Moses. Fab Moses hucheza sarakasi, huimba na kucheza ngoma. Mpiga ngoma maarufu aliyekuwa zamani na Remmy Ongala, Saidi Kanda kashika marimba. Marimba ya Kitanzania ndiyo. Vitu vyetu hivyo.


Kitoto tunapiga mashairi, ngoma na kuicheza. Hapa ni usiku wa kusaidia fedha za kupunguza ukeketaji Tanzania, London, 2014. Ngoma oyee!


Ngoma. Ushirikiano au “jam” baina ya wanamuziki wa Morocco, Argentina na Tanzania. Al Habib hapa anatongoa utenzi wa mshairi maarufu wa Marekani aliyetetea haki za watu weusi Marekani miaka zaidi ya 60 yaani Amiri Baraka au Leroi Jones. Ngoma!!!!
Ngoma. Ukumbi wa Rich Miz, London. Mseto wa wanamuziki toka sehemu mbalimbali za dunia. Huyu dada ana damu ya Kiarabu na Kiafrika na Kizungu. Mpenzi wa ngoma. Mapenzi ya ngoma….
PENDENI NGOMA ZETU JAMA
TUACHE KUIGA IGA MAPIGO YASIYO YETU
SISI MATAJIRI WA LUGHA YA SANAA.

Ngoma. Ndiyo maana wengi,watoto kwa wazee, wanataka na wanapenda kujifunza Ulaya. Ngoma ni kioo, roho na joho letu Waafrika. Utajiri wetu. Ladha.
TUSIPOANGALIA TUTAIPOTEZA NGOMA ICHUKULIWE NA WAGENI WANAOIHUSUDU.

No comments: