ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, February 7, 2015

RAIS KIKWETE AONGOZA MAZISHI YA BI.TAJIRI TANGA

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Bi.Tajiri Abdallah Kitenge wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga.Marehemu Bi.Tajiri ni mama wa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bwana Rashid Othman.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bwana Rashid Othman wakati wa mazishi ya Mama yake Bi.Tajiri Abdallah Kitenge yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga jana(picha na Freddy Maro)

1 comment:

Anonymous said...

inna lillahi waina illahim rajiun kila mmoja atafika mwisho wa safari yake hapa duniani na kwenda kulala hapo chini.hajalishi nani tajiri nani msomi nani fukara,mbumbubu inajojalisha ni amal(matendo yako mema) yako uliyoiete hapa duniani kesho ndo yatakuja kukufaaa.

tumuogope sana Allah na kuacha yale maovu asiyoyataka hii dunia tunapita njia tu tuko safarini hajutafika mwisho wa safari yetu,usieno raha na kila aina ya starehe haba duniani ukaja ukamkosea muumba wango na kupata kibri(jeuri).

tumeumbwa kwa udongo na tutarudi sote kwa udongo huo huo .binadamu hatu na kitu bwana tusijidanganye.

inna lillahi waina illahim rajiun. Allah amlaze mahali pema peponi mzee wetu,mama yetu,ndugu yetu bibi yetu,Ameen ameen ameen thuma ameen.

poleni sana wafiwa wote,ndugu jamaa wana familia,marafiki namajirani na watanzania wote kwa ujumla.

tusisahau hii ndo njia yetu sote tutapita leo mzazi wetu katuacha kesho inaweza ikawa mimi au wewe je umejiandaje.si kutishana ila tujiandae na kukaa vema hapa duniani kwa kumridhia Allah ili siku yetu ikifika atupokea vema.Ameen ameen ameen thuma ameen.

mtanzania aliyeguswa na kila kifo cha mtu/binadamu yeyote yule hapa duniani.