Gardner G Habash na Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ siku ya harusi yao.
BAADA ya wiki iliyopita aliyekuwa mke wa mtangazaji wa kituo cha radio cha EFM, Gardner G Habash, mwanamuziki Judith Wambura Mbibo ‘Lady Jay D’ kumwaga sababu za kuachana na mumewe huyo, mkali huyo wa kutangaza ameibuka na kusema amechukizwa na maneno yaliyotolewa na aliyekuwa mwandani wake huyo huku akidai anamuachia Mungu.
Ishu hiyo iliyopata nafasi kwenye vyombo mbalimbali vya habari, ilitokana na Jide kuwapa watu nafasi mashabiki wake kumuuliza maswali katika mtandao wa kijamii, ambapo asilimia kubwa walitaka kujua kama kweli ameachana na mume wake au la.
Magazeti Pendwa kutoka Global Publishers yakaamua kumtafuta Gardner ili aweke bayana juu ya suala la ndoa yao kutokana na mwanamuziki huyo kuweka wazi kwamba tayari ndoa yao ilikwishasambaratika.
“Alichokisema na ulichokisikia ndiyo ukweli wenyewe. Hakuna ndoa tena, tumekwishaachana na kila mmoja kuchukua kilicho chake. Ila kila kitu namwachia Mungu na wala sina kinyongo naye,” alisema Gardner.
...Wakiwa kwenye pozi.
Siku chache zilizopita mwanamuziki Jide alifunguka kwamba hakutaka tena kuendelea kuishi na mume wake kutokana na tabia mbaya alizokuwa nazo mwanamume huyo, hali iliyomfanya kuishi pasipo kuwa na furaha katika kipindi kirefu cha ndoa yao.
Akifunguka zaidi, Jide alisema kwamba alichoshwa na tabia hizo ambazo alipobanwa zaidi ili aziweke wazi tabia hizo, alisema kwamba mwanamume huyo alikuwa na tabia ya kuwashikashika wanawake kila alipokuwa jukwaani akiimba.
Alipenda kuwatongoza wanawake wengi tu ambapo kuna siku alimkuta akimshikashika mapaja mwanamke ndani ya mghahawa wake, na alipomuuliza, alikiri kufanya hivyo na kuomba msamaha.
Wawili hao walifunga ndoa Mei 14, 2005, jijini Dar es Salaam ambapo mpaka wanaachana, hawakubahatika kupata mtoto.
Credit:GPL
6 comments:
ushauri wa bure, mwanamke kama unataka ndoa yako idumu mchunguze kabla hujaolewa na huyo mpenzi wako wa kiume ni wa aina gani na wazazi wake ni wa aina gani ukisha ridhika naye ndo uoane naye, hakuna love kwenye ndoa ila maelewano tuu,wengi wanao olewa wanaolewa kwa vile wamekubali kuolewa na waliopendwa wengi hawaolewi na hao wanaume so aliye tayari kuolewa ndo anaolewa si kwamba kapendwa sana au kazimikiwa sana no no no.alikuwa yupo tayari kuolewa.
wengi wanakuja kupendana wanapo oana.
chunguza hilo buzi lako ni la design gani,na huko kwao wakoje utapata jibu sahihi uingiye kichwa kichwa ndani ya ndoa hiyo naye ua laaa.
ushauri wa bure kwa yule yule.
nawasilisha.
radhid chiz benz ni kidaga tena kibuwa kidogo sana wako mapapa manyangumi mbona hawakamatwi?
mkulu ana list ya wauza unga wakubwa mbona kakalia tuu.
mwenye akili atajiuliza haya wanaotumia vichwa vyao watajua ukweli wa mambo.
Ukimchunguza bata na miendo yake katu humli. Na kuku wa kienyeji hata atengewe vipi kuchakura haezi acha
ukiona mwanaume anataka kuoa wakati hana hata stable job jua imekula kwako. na kwa marekani ukiona mwanaume anataka kuoa hata paper hana (mwanamke anazo) hapo jua jamaa anataka pepa tu. wanaume wengi wanaoa kwa malengo
Jamani wanaume wa siku hizi wamekuwa ovyoooo sio kama enzi za wazazi wetu walikuwa wanajua responsibility zao ni kutunza mke na watoto siku hizi wanaume wanapenda sana kutunzwa na wanaume,badilikeni jamani wanaume
Sidhani km ni wanume tu, hata wanawake pia wana mambo. Kwani huyo dada wakati anaanza uhusiano na huyo kaka, hakuwa na mke? Ndoa yake kabla ya kumwoa JayD ilivunjikaje huyo kaka? kwa hiyo alimfahamu fika huyo kaka kwa tabia zake za kubadiri wanawake.
Post a Comment