Wednesday, March 11, 2015

ABIRIA 42 KATI YA 67 WAFA AJALI YA IRINGA

Miongoni mwa manusura 22 wa ajali ya basi la Majinja lenye namba za usajili T438 CED wakiwa wamelazwa katika hospitali ya Mkoa Iringa kwa matibabu. Abiria 42 walipoteza maisha katika ajali hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Barabarani mkoa wa Iringa, Salim Asas Abri (kulia) akiwa na viongozi wengine wakiwajulia hali manusura wa ajali hiyo.
Kontena lilokuwa limepajkiwa katika lori la mizigo Scania namba T 689 APJ, mali ya Cipex Company likiwa limelalia juu ya basi lenye namba za usajili T438 CED, mali ya kampuni ya Majinja na kusababisha vifo vya watu 42 na wengine kadhaa kujeruhiwa jana katika eneo la Changarawe, nje kidogo ya mji wa Mafinga mkoani Iringa leo.
Foleni ya magari katika eneo la Changarawe baada ya ajali hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (wa pili kulia) akiwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Ramadhan Mungi ,Mwenyekiti wakamati ya Usalama Barabarani mkoa wa Iringa Salim Asas Abri (wapili kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Mboni Mhita eneo la ajali. 

MAJINA YALIYOPATIKANA HADI SASA NI: Baraka Ndone (dereva), Yahya Hassan ( kondakta), Ester Emanuel, Lusekelo Enock, Jeremia Watson, Digna Solomoni, Frank Chiwango, Luteni Sanga, Teresia Kamingage, Dotto Katuga, Ester Fidelis, Paulina Justine, Mbamba Ipyana, Catherine Mwate, Mwajengo, Ndulile Kasambala, Zera Kasambala, Rebeka Kasambala, Shadrack Msigwa, Mathias Justine, Juliana Bukuku, Cristina Lyimo, Martin Haule na Dominick Mashauri, Omega Mwakasege.

Wengine ni Ester Willy, Lucy Mtenga, Erick Shitindi, Edwiga Kamiyeye, Frank Mbaula, Mustapher Ramadhani, Kelvin Odubi, Upendo William, Charles Lusenge, Neto Sanga, Pili Vicent, Daniel, Jacob Doketa Iman Mahenge , Juma Sindu, Dk A. Shitindi, Six Erick, Frank Mbaule,

Wengine waliokuwepo katika ajali hiyo wametambuliwa kwa jina moja Amadi, Musa, Elias, Raphael, Hussein na Oswald.

Basi hilo lilianza safari mjini Mbeya likiwa na abiria 37.

Picha na habari kwa hisani ya Father Kidevu Blog

No comments: