ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 20, 2015

AJALI YA MIKUMI WATU 7 WALIPOTEZA MAISHA

 Ajali ya mabasi iliyotokea jana Mikumi
Watu saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 48 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Msanga Line walilokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso na basi la Luwinzo katika eneo la hifadhi ya taifa ya Mikumi, wilaya Kilosa, Morogoro.

Ajali hiyo ilitokea jana saa 6:45 mchana, baada ya basi la Msanga Line linalosafiri Dar es Salaam kwenda Mahenge, wilayani Ulanga, Morogoro kugongana na basi la Luwinzo lililokuwa linatoka Njombe kwenda Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Morogoro, Leonard Poul (pichani), chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa madereva wa mabasi yote ambayo walishindwa kuyamudu.

Alisema majeruhi wengi wa ajali hiyo wamelazwa katika hospitali ya Mtakatifu Kizito wakisubiri utaratibu wa kupelekwa katika Mospitali ya mkoa wa Morogoro.

Alisema miili ya marehemu haijatambuliwa na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo.
CHANZO: NIPASHE

No comments: