Advertisements

Friday, March 20, 2015

TEMBA PHOTO NA VIJIMAMBO INAMASIKITIKO MAKUBWA KUWAAMBIA ILE SHOW YA YAMOTO MEMORIAL WEEKEND HAITAKUWEPO


Temba Photo na Vijimambo Media & Entertainment inamasikitiko makubwa kuwataarifu wadau wake kwamba lile Tamasha la bendi ya Mkubwa na Wanae (Yamoto) lililokua lifanyike New York na Washington, DC May 22 na 23, 2015 sasa halitafanyika kutokana na poromota mwingine wa Marekani kuingilia kati baada ya kuona Tangazo kwenye Vijimambo kwamba Temba Photo wakishirikiana na Vijimambo Media & Entertainment inawaleta Yamoto Band.

Maongezi ya Yamoto Band yaliyofanywa kati ya NY Ebra na Meneja wa kikundi hicho bwn. Said Fela na kukubaliana gharama zao za kufanya maonesho New York na Washington, DC na kilichokua kimebaki ni taratibu za kuwaombea VISA ya Kazi na hatimaye waweze kuja na kutoa burudani kwa wadau na wapenzi wa kikundi hicho nchini Marekani..

Chakushangaza ni tangia juzi kati Ny Ebra alipompigia simu Bwn. Said Fela, hakutoa tena ushirikiano wa kutosha na kumweleza kuwa ameongea na poromota mwingine wa huku Marekani na kumtaka waje mwezi wa April badala ya onesho letu lililokua lifanyike mwezi May na cha kusikitisha poromota huyo akamwambia aatueleze tumpigie simu pamoja na kwamba hicho hakikua makubaliano hapo mwanzo hata hivyo Ny Ebra alimpigia simu huyo poromota mara kadhaa lakini hakupokea simu yake.

Jana Jumanne March 17, 2015 NY Ebra alijaribu kumpigia Bwn. Said Fela kutaka kumjulisha kwamba poromota wake hapokei simu. Bwn. Said Fela hakuipokea simu yake. Leo March 18, 2015 NY Ebra alimvutia waya tena Siad Fela lakini Meneja wa kikundi cha Mkubwa na Wanae ilishaonesha ameishajazwa pumba nyingi ndipo NY Ebra kwa niaba ya Vijimambo na Temba photo aliamua kubwaga manyanga na kusikitika na tabia maji taka aliyofanya poromota huyo ambayo anapokua na onesho au shughuli moja wapo Vijimambo na Temba photo uheshimu shughuli yake. Hii sasa ni kuvuka mipaka na Vijimambo na Temba photo tunalaani vikali tabia kama hii.

Mwisho tunawaomba radhi wadau wetu na tunaagalia kwa sasa ni msanii gani mwingine tumlete kwa ajili ya kutoa burudani na kukata kiu yenu ya muda mrefu.

Vijimambo na Temba photo inawatakia kila la kheri Yamoto Band kwa onesho lenu Marekani

Asante

Uongozi Timu Vijimambo kwa ushirikiano na Temba photo.