ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 3, 2015

Balozi Seif akabidhi vifaa vya ujenzi jimboni

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi vifaa vya ujenzi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Tawi la Chama cha Mapinduzi Kwa Gube Mfenesini.

Kulia ya Balozi Seif ni Mwenyekiti wa CCM wa Tawi la CCM la Kwa Gube Ndugu Salum Ali Mzee.
Balozi Seif akizungumza na Wana CCM wa Tawi la Kwa Gube mara baada ya kukabidhi vifaa kuendeleza ujenzi wa Tawi hilo.

Kushoto yake ni Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi, Mwenyekiti wa Tawi la CCM Kwa Gube Nd. Sal;im Ali Mzee na kulia ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Kamati ya Siasa ambaye pia Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “ B” Nd. Haji Makungu Mgongo.
Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif akimkabidhi vifaa vya ujenzi Katibu wa Maskani ya CCM ya Mtakuja iliyopo Kazole Bibi Zena Issa kwa ajili ya uendelezaji ujenzi wa Maskani hiyo.
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kitope Mama Asha Suleiman Iddi akiwashauri wana CCM, wa Matawi ya Jimbo hilo kuanzisha madarasa ya maandalizi ili kuwaondoshea usumbufu wa elimu watoto wao.

Kushoto ya Mama Asha ni Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
Balozi Seif Ali Iddi akimkabidhi vifaa vya Ujenzi Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Msingi ya Matetema Kazole Mwalimu Ali Salim Ali ili kusaidia kuendeleza ujenzi wa jengo la pili la Skuli hiyo.

Picha na – OMPR – ZNZ.

Na Othman Khamis Ame, OMPR

Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba juhudi za Wananchi wa Vijiji vya Matetema na Kwa Gube Mfenesini ndani ya Jimbo la Kitope za kujenga Skuli sambamba na ongezeko na Madarasa linafaa kuungwa mkono na jamii.

Alisema kitendo cha wananchi hao kwa kiasi kikubwa kitaleta ukombozi kwa watoto wao hasa wale wa umri mdogo wa kufuata elimu katika Vijiji vya mbali masafa ambayo wakati mwengine yanawasababishia hatari ya maisha yao wakati wa kuvuka bara bara.

Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza hayo wakati akikabidhi vifaa vya ujenzi kwa Uongozi wa Skuli ya Maandalizi ya Kwa Gube Mfenesini waliyoanza kwa hatua ya msingi wa jengo la Maandalizi pamoja na ule wa Skuli ya Matetema unaoendelea na ujenzi wa jengo la Pili.

Vifaa vilivyotolewa kutokana na fedha za mfuko wa Jimbo ni Matofali elfu 2,600 kwa skuli ya Maandalizi Kwa Gube ambapo Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini “ B “ imeonyesha nia ya kusaidia saruji, wakati Skuli ya Matetema ikakabidhiwa matofali 1,500, nondo,saruji fedha za fundi vitu vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 5,425,000/-.

No comments: