ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 3, 2015

TANGAZO MAALUM

  

 NAFASI ZA WAALIMU WA KUJITOLEA KUFUNDISHA KISWAHILI

Madarasa ya Kiswahili huendeshwa kila Jumamosi ;
White Oak Community Recreation Center 1700 April Lane, Silver Spring, MD 20904  MUDA: Kuanzia saa 9 mchana hadi saa 11 Jioni.
             
MALENGO:
  • Kufundisha kuongea na kuandika kwa lugha ya Kiswahili kwa waTanzania na marafiki zao hapa Washington DC, Maryland na Virginia.
  • Kufundisha Utamaduni unaoendana na kujifunza lugha ya Kiswahili.
  • Kujenga jamii iliyo imara kwani lugha ni kiunganishi chetu.
SIFA ZA MWOMBAJI: 
  • Mtu yeyote anayeweza kuongea na kuandika lugha zote mbili kwa ufasha (Kiswahili na Kiingereza).
  • Mtu yeyote mwenye uwezo wa kujitolea muda wake (wikiendi mbili) kusaidia watoto na watu wazima kujifunza lugha ya Kiswahili.
  • Mtu aliye na uvumilivu.
  • Mtu yeyote mwenye uwezo wa kutayarisha somo na kutahini wanafunzi wa lugha ya Kiswahili.
  • Mtu yeyote anayeelewa mila na desturi ya watu wanaozungumza Kiswahili.
  • Mtu asiye na kizuizi cha kuwepo katika mazingira ya watoto 
MAAGIZO
Jumuiya ya watanzani inatoa vitabu na inafuata mfumo wa kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni hapa Marekani.

FAIDA YA KUJITOLEA KUFUNDISHA
  • Jumuiya ya Watanzania DMV inatoa msaada wa kukuwezesha kujiendeleza kwa kupata elimu na cheti cha kuwa mwanataaluma wa kufundisha Kiswahili hapa Marekani.
  • Jumuiya inatoa vitabu vya kufundishia.
  • Jumuiya inasaidia kutoa barua za kumbukumbu zako binafsi kwa kazi zote za kujitolea ulizozifanya katika ufundishaji wa Kiswahili na kutumia barua hiyo kupata ajira katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili.
    MAENDELEO YA KWELI HULETWA NA HUDUMA YA MWANANCHI  KWA JAMII .

                                                   TUNATANGULIZA SHUKRANI.

2 comments:

Unknown said...

mimi ni sekela alphonce mwakyusa, ninasifa za kufundisha kiswahili kwa kujitolea,je maombi yangu nitume wapi? msaada tafadhari. Alphoncesekela@yahoo.com

MARIA FONGA said...

mimi ni Mary Fonga, ninasifa ya kufundisha Kiswahili kwa kujitolea, je, maombi yangu nitume wapi?

mawasiliano yangu ni 0654342569 au maryfonga@gmail.com