Na Henry Mdimu
Tangu asubuhi leo nilikuwa busy na awareness za uwanja wa Taifa katika mechi ya watani wa Jadi Yanga na Simba (picha ya pili). Ila jioni hii nilipoangalia simu yangu nikakuta watu wakinilaumu kutokana na tukio la mtoto Baraka Cosmas (picha ya kwanza) ambaye usiku wa kuamkia leo amekatwa mikono yake.
Wanasema nilikuwa nakula Bata Uwanja wa Taifa huku watu wanateketea.
Hasa alikuwa akiongea mtu anaitwa @hmgeleka.
Kwanza nalaani kitendo hicho cha kikatili na kuzidi kumuomba Rais wangu Mhe Jakaya Mrisho Kikwete aongee na vyombo vyake vya usalama, wasiliache hili lipite hivi hivi.
Lakini jingine jamani suala hili sio la mmoja. Kwa sababu nimejitwika ubalozi ndio nilaumiwe kwa hata lililo mbali na mimi?
Vita hii ni ya wote, mimi nina wiki mbili tu tangu nianze kazi hii na bado natafuta mtaji wa kuendesha zoezi langu.
Tafadhali tutende wote tusinyoosheane vidole, huku tukiwa vijiweni, mmenielewa?
#IMETOSHA
Bango la harakati za "Imetosha!" likiingizwa uwanjani sambamba na ya FIFA ma FIFA Fair Play wakati wa mchezo wa ligi kuu wa watani wa jadi Simba na Yanga Uwanja wa Taifa leo. Chini ni Balozi wa Harakati za Imetosha Henry Mdimu akiongea machache kuhusu harakati hizo zenye lengo la kuhamasisha wadau wote kukomesha vitendo vya mauaji na vya kikatili dhidi ya ndugu zete Albino.
Wachezaji wa Yanga na Simba wakiingia uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam wakiwa wamevaa fulana maalumu za harakati za "Imetosha!"
Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani
Marafiki wa harakati za "Imetosha!" wakisubiri kuingia uwanjani. Marafiki hao ni mchanganyiko wa wana habari, bloggers, wasanii na wanaharakati wengine
3 comments:
Jamani achene huu ukatili kwa watoto na watu wote wanaolengwa. Mnakuwa km hamkuzaliwa na binadamu, je, ktk family zenu wakizaliwa alibino mtawakata viungo pia? Ni aibu na uchungu mkubwa kwetu kwa mnayoyafanya. Umasikini wa fikira mlionao unasababisha makovu ya machungu kwa hawa binadamu mnaowawinda. Nyerere angelikuwa hai labda angeshalitafutia ufumbuzi hili swala. Mshindwe ktk jina Yesu!
Ikiwa ni wapinzani wanataka kuandamana utaona serikali inatuma vikosi vya usalama mara moja kuwatawanya watu LAKINI SUALA LA MAUAJI YA ALBINO NI POROJO TU HAKUNA VITENDO SASA HUYU MTOTO NI WANGAPI TANGU MAUAJI HAYA YAANZE?????
SHAME ON YOU JK AND YOUR GOVERNMENT...!!!
Na hii ndiyo taabu ya kuchagua viongozi waswahili swahili tu.
Henry, you are doing a great job, God bless you!
Post a Comment