Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Katibu Mkuu Ban Ki Moon, wakifurahia jambo walipokuta katika moja ya mikutano ya kimataifa. Akielezea nini kilichosababaisha vuguvugu hilo la kila mwanamke, kila mtoto kuwa na mafanikio makubwa.Ban Ki Moon alisema utashi wa kisiasa na utayari ulioonyeshwa na viongozi mbalimbali akiwamo Rais Jakaya Kikwete ndio baadhi ya sababu zilizochangia kufanikiwa kwa mkakati huo. Rais Kikwete akiwa mwenyekiti mwenza na Waziri Mkuu wa Canada walisimamia Kamisheni ya Habari na Uwajibikaji baada ya kuombwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, jukumu ambalo wamelitekeleza kwa ukamilifu na kutoa mchango mkubwa katika uboreshaji wa afya ya mama na mtoto kupitia vuguvugu hilo la kila mwanamke, kila mtoto.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon akizungumza siku ya Jumanne, wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu mkakati wa kimataifa wa kila mwanamke, kila mtoto ambao Ban Ki Moon aliuanzisha mwaka 2010. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa vuguvugu hilo ambalo kwa ushirikiano baina ya wadau mbalimbali zikiwamo serikali, mashirika ya kimataifa, asasi zisizo za kiserikali, wasomi, wanaharakati na sekta binafsi zimewezesha kuokoa maisha ya wanawake na watoto 2.4 milioni.
Na Mwandishi Maalum.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon,
amesema kama si utashi wa kisiasa,
kujituma, na kujitolea kulikofanywa na
viongozi mbalimbali aliowaomba kufanya naye kazi kwa karibu huku wengine
wakijitolea wenyewe, uhai wa wanawake na watoto 2.4 milioni
usingeokolewa.
Ban Ki Moon ameyasema hayo siku ya Jummane wakati wa uzinduzi wa ripoti mpya kuhusu mkakati wa kimataifa kuhusu vuguvugu la
kila mwananamke, kile mtoto, ( every woman, every
child) mkakati ambao Ban Ki Moon aliuratibu mwaka 2010 .
“ Siri kubwa ya mafanikio ya
mkakati huu ni uwajibikaji. Nilipoanzisha mkakati huu niliwaomba baadhi
ya viongozi wanisaidie, wapo waliosaidia katika uhamasishaji wa raslimali fedha, wapo kama Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania na waziri Mkuu wa Canada
ambao walisimamia suala zima la habari na uwajibikaji, mchango wao, kujituma kwao na uthubutu wao
ndiyo umetufikisha hapa , tumeweza kuokoa maisha ya wanawake na watoto wengi na kazi bado inaendelea”
ameeleza Katibu Mkuu
Akasema mkakati huo
aliouzisha wa kila mwanamke, kila mtoto na ambao chimbuko lake ni lengo namba nne na tano la maendeleo ya millennia ni
mkakati ambao si tu umekuwa wa mafanikio makubwa lakini umegusa hisia za wadau mbalimbali za watu wengi .
Malengo namba nne na
tano ya maendeleo ya millennia na ambayo yanafikia ukingoni mwisho mwa
mwaka huu yanajikita katika
kupunguza idaidi ya vifo vya wanawake na idadi ya vifo vya watoto chini ya
miaka mitano.
“Nilianzisha mkakati huu kwa sababu mimi mwenyewe nimeguswa katika
maisha yangu utoto wangu kwa kuondokewa( kufariki) kwa kaka na dada zangu kwa
matatizo ambayo yangeweza kuzuilika.
Simulizi alizokuwa akisimuliwa na
mama yake juu
hofu kuu wanayokuwa nayo wanawake wanapokwenda kujifungua vile vile ni
moja ya hamasa iliyonifanya nianzishe mkakati huu. Lakini pia katika utekelezaji wa majukumu
yangu nimekutana na visa vingi vilivyoongea
nia na ari kuwa
na mkakati huu” ameeleza Ban Ki Moon
Ripoti hiyo ambayo uzinduzi wake umekwenda sambamba na
mkutano wa 59 wa Kamisheni kuhusu hadhi ya wanawake, inabainisha kwa kina mafanikio na changamoto
mbalimbali za utekelezaji wa katika eneo
hilo linalohusu afya ya mama na mtoto.
Ban Ki Moon amesema amefarijika na kutiwa moyo sana
Kwa mfano Makati huo ambao umegusa hisia wa wadu mbalimali wakiwamo viongozi wakuu wan chi na serikali, asasi zisizo za kiraia, wanaharakati na
makampuni binafsi.
taarif yasingeushirikiano wa karibu baina yake na Viongozi wakuu
wa mataifa mbalimbali umesaidia kuokoa maisha ya …………….., ambao wangepoteza maisha yao wakati
wa kujifungua.
No comments:
Post a Comment