ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 5, 2015

BODA BODA MBEYA WATANGAZA MGOMO WA KUTOBADILISHA NAMBA ZA PIKIPIKI


MWENYEKITI wa chama cha Bodaboda mkoa wa Mbeya, VICENT MWASHOMA.
KATIBU wa Bodaboda mkoa wa Mbeya, MSUMBA MDESA, akitoa tamko kwa niaba ya waendesha Boda boda mkoa wa Mbeya.

Mabango yakafuata na kuanza kusema kama yanavyosomeka hapo chini. 
BAADA ya mabango na tamko, wakaonesha wamekubaliana, kisha yakafuata makofi kutoka kwa viongozi wengine ambao walikusanyika leo katika ukumbi wa Coffee Garden Jijini Mbeya.
Baadhi ya viongozi kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya, wakisikiliza wakati viongozi wao wa mkoa, wakisoma tamko kuhusu kugoma kuanzia leo kwenda TRA kubadili namba za BODABODA zao kwa madai kuwa wanalipishwa na gharama ambazo hawastahili huku madarali(matapeli) wakiwa wamejaa ndani na nje ya jengo la TRA ambapo hata elim ya kutosha kuhusu ubadilishaji wa namba hizo, hawajapata.
Kushoto waliosimama ni baadhi ya watangazaji wa redio mbalimbali mkoani Mbeya, wakiwa ndani ya ukumbi wa Coffee Garden asubuhi ya leo.
Baada ya kikao cha Bodaboda mkoa wa Mbeya na kutoa tamko, baadhi kutoka Mbalizi Mbeya, Vijijini, wakahitaji kupiga picha ya pamoja na Mhariri mkuu wa Blog hii ya Kalulunga Media, SAUTI YA WASIO SIKIKA, Gordon Kalulunga, anayeonesha kidole mbele.
Aliyevaa saa mkoano wa kulia ni Mtangazaji wa kituo cha BARAKA FM cha Jijini Mbeya, ndugu Charles Mwaipopo(Malafyale), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Bodaboda Mbeya.
CREDIT:KALULUNGA MEDIA

No comments: