Mada ya wiki iliyopita, Je, Ungekuwa Hujafanyiwa Kitchen Party iliisha kwa pongezi kadhaa huku wengi wakisema wamejifunza kitu. Lakini wapo walionipinga wakisema mada yangu haikuwa sahihi kwa sababu katika uhusiano pande zote zinaweza kusababisha mtu kubadili tabia, nilipokea mawazo yao.
Leo, nimeguswa kuzungumzia mada ya uhusiano. Kwamba, katika maisha, kosea kila kitu lakini mtu asijekosea katika kuchagua mtu sahihi kwenye uhusiano.
NI KILIO CHA DUNIA NZIMA, BONGO TUMO
Nimevutika kuandika mada hii baada ya kugundua kuwa, leo hii wako watu mamilioni kwa mamilioni duniani kote wanalia kwa sababu ya maumivu yaliyotokana na uhusiano. Nazungumzia uhusiano wa kimapenzi.
Katika utafiti wangu wa kina nimebaini kuwa, katika miaka ya kisayansi na teknolojia, ukiwakuta watu kumi, saba wameshalizwa na mapenzi, usalama upo kwa watatu tu!
Hali hii inatisha sana! Wengi wamejikuta wakijutia kuingia kwenye uhusiano, uwe wa bila malengo (kuburudishana tu), uwe wa uchumba au ndoa.
NI MANENO YA MOYONI
Asilimia kubwa ya wanaoteseka katika uhusiano wamejifungia na maumivu ndani ya mioyo yao. Maneno yao kila kukicha ni ‘ningejua...ni kwa nini nilimkubali huyu...ni kwa nini sikumchunguza...’ lakini muda umeshakwenda baba, mama, dada na kaka!
MAUMIVU YENYEWE YALIVYO
Wikiendi iliyopita nilikutana na mdada mmoja akiwa anahuzunikia moyoni baada ya mumewe wa ndoa kubadilika tabia.
Huyu dada alikuwa akitafuta kazi, kwa vile mumewe amekata mawasiliano na familia baada ya ‘kutekwa’ na mwanamke mwingine ‘nyumba ndogo’. Jamani!
“Sikujua kama mume wangu angekuja kubadilika hivi. Kabla ya ndoa tulichunguzana sana, nikamwona ni mwanaume mwenye kujali familia, anawajibika na ndugu wa pande zote, lakini alipokuja kubadilika, hata siamini kama ni yeye.
“Mume wangu niliyempenda kwa dhati naye kuonesha kunipenda kabadilika sana, hajui nakula nini na watoto, watoto wanakwendaje shule au wanatibiwa vipi wanapougua.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba hata watoto wanapomuona huko mitaani, wakimfuata na kumsihi arudi nyumbani kwa sababu wanakosa mapenzi yake, huwajia juu utafikiri siye aliyewazaa.
“Kwa kweli inauma sana, kwa asiyefikwa na masaibu kama yangu hawezi kujua maumivu ninayopata baada ya mume wangu kuondoka na kuniacha nikihangaika na watoto.
“Kuna wakati nahisi yule mwanamke mwizi wangu amemchezea mume wangu. Haiwezekani mume aondoke nyumbani na begi la nguo tu na kuacha kila kitu.
“Mbaya zaidi nasikia kule kwa mwanamke alipo, ni chumba kimoja tu na ndiyo sebule pia. Mimi hapa kaniacha kwenye nyumba ya vyumba vitatu, sebule, jiko, bafu, choo na stoo. Ama kweli nimeamini nilipoambiwa kua uyaone, siyo majengo,” alisema mdada huyo, mkazi wa Kimara-Temboni, Dar.
NINI HUTOKEA?
Ni dhahiri kwamba, katika uhusiano kila mmoja aliyemkubali mwenzake aliamua kutoka moyoni kwamba ndiye chaguo lake.
Wengi walidiriki kugombana na ndugu zao, marafiki au hata kukejeliwa kwa sababu ya kuwa na uhusiano na mtu f’lani lakini kwa sababu aliona ndiyo chaguo lake aliamua liwalo na liwe.
Watu wa kundi hili, inapotokea kuumizwa kimapenzi hulia sana kuliko mtu aliyefiwa. Kilio kikubwa kinatokana na kumbukumbu za kuonywa, kupoteza vitu au kuharibu uhusiano ili ampate ampendanye ambaye aliona ni chaguo lake.
TATIZO LIKO HAPA SASA...
Tukutane wiki ijayo usikose.
GPL
No comments:
Post a Comment