MASHEIKH wapatao 50 kutoka Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani, leo wamemkabidhi kiasi cha shilingi 700,000/- za kuongezea kuchukua fomu ya kuwania urais 2015. Mashekhe hao wakiongozwa na Yusuf Surulu (kulia) na Alli Mtumwa (wapili kulia) wamemkabidhi fedha hizo nyumbani kwake mjini Dodoma na kushuhudiwa na Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof Juma Kapuya.MSIKILIZE HAPA.
Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, wamesema katika salamu zao kuwa wameona mtu pekee anayefaa kushika wadhifa huo ni yeye (Lowassa) hivyo wanamsihi atangaze nia na achukue fomu ya kugombea na wapo nyuma yake katika dua.
Lowassa amewaambia viongozi hao wa dini kuwa makundi mbalimbali ya jamii yamekuwa yakimuomba kugombea Urais lakini wao wamemfanya ashawishike sasa kufanya hivyo wakati ukifika.
"Ila nataka kuwaahidi, naheshimu sana maneno yenu na nayakubali kwamba siku ikifika kwa taratibu za chama nitachukua fomu,"alisema.
Lowassa amesema endapo Mungu atamjalia kushinda uchaguzi, atahakikisha anaendeleza pale Rais Jakaya Kikwete katika nyanja mbalimbali za Elimu, afya kilimo kwanza, na huduma nyingine muhimu kwa jamii.
Lowassa amesema akifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu.
Lowassa amesema akifanikiwa nitaanza na elimu, na kufanya elimu kipaumbele chetu kwani elimu ndio msingi wa kila kitu.
Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akiwa amepokea fedha zilizo changwa na Mashekhe kutoka Wilaya ya Bagamoyo. Walio mkabidhi fedha hizo ni Shekhe Yusuf Surul (kulia) na Ally Mtumwa. Mwingine ni Mbunge wa Urambo Magharibi, Prof. Juma Kapuya.
MASHEKHE hao wakiwasili nyumbani hapo kwaajili ya mazungumzo na Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa akiwasikiliza viongozi wa msafara huo.
Edward Lowassa akizungumza na Mashekhe hao mjini Dodoma.
Mashekhe hao kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Bagamoyo, Mlingotini, Kaole, Chalinze, Lugoba, Msata na kwingineko.
Duaa ilisomwa na viongozi hao wa dini.
Edward Lowassa akiwasindikiza viongozi hao.
Lowassa akiagana na Sheikh Alli Mtumwa mmoja wa viongozi wa msafara huo.
Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa akiagana na viongozi hao.
Lowassa akimsikiliza mmoja wa Mashekhe hao.
9 comments:
Wow. Umaskini utawamaliza Watanzania
Heheeeee....kampeni za kibongo ni nomaaaaa...yani mashekhe wampe lowasa laki Saba agombee, na wakati huko bagamoyo Kuna watu wanakufa njaa,,hata mlo mmoja kwa siku hawaa.heheeee kweli hiki ni kiini Macho.
WaTanzania umefikia muda wa kuchambua ipi Pumba na Ipi mchele!! Kumekuwa na makundi ya aina mbalimbali kuanza kufanya hizi kampeni za kumshawishi na kumtala mhe. LOWASSA atangaze kugombea Urais!! Je ile mikataba hewa haitaendelea kutafutwa tujue kuwa tumerudi nyuma kiasi cha kutosaha kuna umuhimu wa kusonga mbele na tunajua anaweza lakini basi tumpeni cheo kingine ndani ya nchi hii!! WaTanzania kazi kwetu..
HUU ni mchezo wa kuigiza haungii akilini, hawaa sio masheikh bali ni waganga au wafanya tiba wameenda Dodoma kwa kazi maalumu ya kufanya dawa ili Lowasa akubalike katika kamati kuu ya CCM,tujiulize kwanini Lowasa alazimishe kuwa rais ana biashara gani Ikulu?
Mashekhe 50 waende Dodoma nauli na Hotel anawalipia nani? pia watoe laki 7,wakati Tsh.700,000= ni matumzi ya chakula cha mifugo ya Lowasa kwa siku!
Hivi kweli Msikiti au Siasa na dini vinaingiliana? au Msikiti na viongozi wake wawe ni sehem ya vyombo vya kampeni za Lowasa? hawa sio masheikh ni wanafiki na hakuna mwislamu yeyote nayekubaliana nao, bali njaa yao inawasumbua
Only in Tanzania mtu anaachishwa kazi kwa ufisadi na ubadhirifu wa mali za umma mtu huyo huyo leo anagombea uraisi. Cycle of poverty huu ndio ujinga Msuya alikuwa anazungumzia juzi mnachagua viongozi wabovu badae mnalalamika nchi maskini
Mbona ni Lowassa pekee ndie anakampeni ? Au CCM washaamua ? Upinzani nako CHADEMA hakuna kitu
Mbona mkewe lowassa hasikiki yaani hamfanyii mumewe kampeni,yaani anataka aje kuwa first lady kirahisi hivyo kafunga mdomo tuu yatamshinda hamkuona mama Obama alivyofanya mchakamcha ndiyo akaweza kuingia white house. Mama changamka
Sasa hawa waganga wa kutabiri nyota au unajimu leo wamekula fedha za Lowasa kesho kwa mungu wataelezea nini? kuna matatizo au changamoto ngapi zinaikabili taasisi za kiislam ,pamoja na shule,madrasa na juzu za kusomea leo hii hawa wazee walipe nauli kwenda Dodoma,hii ni Bongo Move
Hii ni msg kwa Lowasa yani mzee umekuwa haujiamini kiasi utumie vyombo vya Ibada ??Kiongozi gani anafanya hivyo??watanzania mnachaguwa kiongozi aliwaibia kwa uwaziri mkuu kwa mda mchache mnataka kumpa urais miaka kumi na nchi mmesikia sasa ni tajiri kweli mnajuwa mnachokifanya Au mnaangalia viabasha vya siku moja??Watanzania wacheni kujiabisha nyie viongozi wa fini au Waganga wa jadi??
Post a Comment