Advertisements

Friday, March 27, 2015

MAAFA MINGINE NEW YORK CITY

Maafa haya yametokea New York Friday na kusabaisha watu 22 majeruhi na watu wawili kupotea hadi sasa hawajulikani walipo. Inasemekana Gas ndani ya restaurant ndiyo ilisababisha maafa ya moto huu ulioteketeza  majengo matatu  pamoja na restaurant ya Sushi Park kwenye barabara ya 2 maeneo ya East Village New York majira ya saa tisa jioni na kusababisha shughuli za maeneo hayo kusimama na watu kukimbia ovyo. Inasemekana mmiriki wa restaurant hiyo alisikia harufu ya gas dakika 15 kabla ya moto kutokea na kuchelewa kutoa taarifa na pia kifaa cha carbon monoxide kilikuwa kimekufa.

Vikosi vya zima moto vikiwa kazini kujaribu kupunguza kasi ya moto huo.
Ikumbukwe ni wiki mbili tu tangu moto mwingine uliuwa watoto 7 wa familia moja maeneo ya Brooklyn New York.


No comments: