Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja, jana alimkemea mbele ya waathirika wa mvua ya mawe na upepo, Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya, kwa kushindwa kuwajibika na kuwasababishia watu hao kukosa chakula.
Zaidi ya waathirika 250 waliopata hifadhi katika Shule ya Msingi Mwakata wilayani hapa, walishinda njaa licha ya chakula cha msaada kuwamo ndani ya darasa, lakini walishindwa kupewa kutokana na uongozi wa serikali kutokuwapo maeneo hayo.
Mgeja aliyewasili katika kambi hiyo akiwa amefuatana na Mbunge wa Jimbo la Msalala, Ezekiel Maige, walipokelewa na vilio toka kwa akinamama na watoto waliokuwa na njaa.
Hali hiyo ilisababisha Mgeja kumpigia simu Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Allynasoro Rufunga, na kumfahamisha jinsi waathirika hao wanavyolia kutokana na kutopewa chakula kwa wakati.
Hata hivyo, baada ya dakika chache Mkuu wa Wilaya (Mpesya) akiongozana na baadhi ya viongozi wengine wa wilaya, walifika eneo la tukio na kumkuta Mbunge Maige akiwagawia chakula waathirika hao.
“Nyie wanasiasa hamtakiwi kuingilia masuala haya, siasa na majanga wapi na wapi,” Mpesya alionekana kuongea kwa kejeli.
Kutokana na kauli hiyo, Mgeja alimtaka mkuu huyo wa wilaya kuacha kufanya dharau kwa jambo kubwa kama hilo, kwani wananchi waliokuwa wakilia njaa, ni miongoni mwa walioiweka CCM madarakani.
“Hili tukio ni la wote, hizo kejeli zako hazifai kuzileta hapa kwani bila viongozi wa chama hiki kuwapo madarakani usingeipata nafasi hiyo…kwanza wewe si saizi yangu wa kubishana, mie nipo kitaifa zaidi,” alisema Mgeja huku akiwa amekasirika.
Hata hivyo, mkuu wa mkoa Rufunga, aliyewasili baadaye katika tukio hilo, alisema Mgeja alikuwa sahihi kwani ndiyo moja ya kazi yake kutokana na chama anachokisimamia kuongoza nchi.
“Mgeja ana jukumu la kuwakemea viongozi wa serikali kutokana na chama anachokiongoza kuwaweka madarakani viongozi wote,” alisema Rufunga.
Kucheleweshewa wananchi hao chakula, kumeenda kinyume na agizo la Waziri Mkuu Mizengo Pinda, aliyewatembelea juzi na kusema chakula na misaada yote, lazima wapewe walengwa kwa wakati.
Katika hatua nyingine, majeruhi 12 bado wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama, kufuatia kuumia wakati wakijiokoa na janga la mvua ya mawe na upepo mkali katika kijiji cha Mwakata usiku wa Jumanne iliyopita.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Joseph Ngowi, akizungumza na NIPASHE jana, alisema kati ya majeruhi 102 waliopokelewa, 87 wameruhusiwa na watatu walifariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.
“Licha ya majeruhi hao kuruhusiwa, lakini changamoto kubwa tunayokabiliana nayo ni wagonjwa wengi kushindwa kuelewa waende wapi baada ya nyumba zao kuporomoshwa na mvua hiyo…lakini yupo msamaria ambaye ni padre amewachukua baadhi yao,” alisema Dk. Ngowi.
Akizungumzia tukio hiyo, muathirika Mbiya Lubisana, aliyelazwa Hospitali ya Wilaya Kahama huku akiwapoteza wazazi wake wote, alisema analikumbuka janga hilo na kushindwa kulielezea licha ya kuumia kiuno, kichwa, na macho.
WANAFUNZI 1000 KUKOSA MASOMO
Wanafunzi zaidi ya 1000 wa Shule ya Msingi Morini, Wilaya ya Kongwa, watakosa masomo kwa muda kutokana na baadhi ya mapaa ya majengo ya shule hiyo kuezuliwa na mvua iliyoambatana na upepo mkali na mawe.
Mvua hiyo iliyoanza kunyesha saa 10 jioni juzi iliezua mapaa ya madarasa mawili, ofisi ya walimu na nyumba ya mwalimu Adrofina Jenga, huku nyumba nyingine za walimu zifurika maji.
Tukio hilo lilithibitishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa, Lilian Matinga, ambaye aliahidi kuwa halmshauri inafanya haraka iwezekanavyo kurejesha hali ya utulivu katika mazingira ya shule hiyo ili, wanafunzi warejee masomoni mapema.
Akizungumza na NIPASHE, Mwalimu wa afya shuleni hapo, Napendaeli Mcharo, alisema mvua iliyonyesha kati ya Saa 10:00 jioni hadi Saa 1:30 usiku iliambatana na upepo mkali ilidhaniwa kuwa ya kawaida lakini ilipofika kati ya muda huo na saa 5:00 iliendelea kuleta madhara hayo.
“Tulisaidiana kuondoa maji ndani ya nyumba ingawa ilikuwa kazi kubwa, kushindana na maji, wenzetu wawili walishindwa kurejea nyumbani kwao kutokana na hali ya hewa ilivyokuwa nje hivyo maji yalijaa ndani ya nyumba zao kwakuwa hatukuweza kuingia ili kuwasaidia kuyatoa nje,” alieleza Mcharo.
Walimu wengine ambao nyumba zao zilijaa maji kiasi cha kuharibu mali zao, ni Adrian Barabara na Mariam Mtana. Aidha, mali za shule ikiwa ni pamoja na madaftari ya wanafunzi, makadirio na maandalio ya walimu, vitabu na nyaraka mbalimbali ziliharibiwa na kusombwa na maji ya mvua.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment