Mama Salma akipungia washiriki wa matembezi wakati wakiwasili viwanja vya Mnazi Mmoja
Wanawake wa Tanzania leo Jumapili Machi 8, 2015, wameungana na wenzao Duniani kote, kusherehekea siku ya Wanawake Duniani. Kitaifa sherehe hiyo imefanyika mkoani Morogoro, wakati jijini Dar es Salaam, wanawake kutoka wizara, taasisi za umma, halmashauri zote za jiji pamoja na vikundi vya wajasiriamali, walishiriki matembezi kutoka jengo la Ushirika barabara ya Lumumba jijini Dar es Salaam, hadi viwanja vya Mnazi Mmoja na kupokelewa na Mwenyekiti wa WAMA, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete. Matembezi hayo yaliongozwa na brass band ya Jeshi la Magereza sambamba na vikundi vya matarumbeta vilivyoletwa na taasisi tofauti. Wanawake huitumia siku hiyo kupaza sauti zao ili kutetea haki na nafasi yao katika jamii.
Wafanyakazi wa PPF, nao walikuwepo na hapa walilazimika kukimbia mchakamchaka badala ya kutembea, yote ilikuwa ni katika shamra shamra za kupamba siku hiyo
Picha kwa hisani ya K-VIS Blog
1 comment:
Ongera"mama salima"kikwete" tembelea kijiji kimoja kiitwacho"kibare" kinapatikana BUKOBA"
Post a Comment