Advertisements

Sunday, March 1, 2015

Mhe. Jussa asema Suala la Katiba mpya halijafikiwa kama Wananchi walivyotarajia

Muwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV Siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall uliopo University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
Na Abou Shatry Washington DC
Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Mhe: Ismail Jussa Ladhu amesema Tanzania inaelekea kusipotarajiwa na maoni ya wananchi waliyotoa maoni.
Aidha amesema matarajio ya watanzania hayajatimizwa mbali ya kuwepo mijadala mingi juu ya rasimu ya Jaji Warioba ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu katika Suala la katiba mpya. Mhe. Jussa aliyasema hayo wakati akizungumza na Watanzania wa DMV siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall 1401 University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
Pia Mhe. Jussa ambaye pia ni mjumbe wa UKAWA amesema uamuzi wa UKAWA kususia na kujitoa katika bunge la katiba ni kwa sababu chama tawala CCM kimekwenda kutetea sera zake na kupinga mawazo ya wananchi ambayo yamewakilishwa katika rasimu ya Jaji Warioba. Mkutano huo ulijumuisha Agenda kadhaaha ikiwemo Mchakato wa Katiba mpya, Ufafanuzi juu ya muundo wa serikali tatu, Uamuzi wa UKAWA kususia mchakato huo dhalimu na sababu ya maoni ya watu walio Diaspora kuhusu Uraia Pacha kutokutekelezwa kama walivyotarajia.

Video ya maswali na majibu utawajia hapo baadae
Watanzania waishio DMV(Washington DC, Maryland na Virginia) wakimsikiliza Mh Ismail Jussa alipohutubia katika mkutano uliondaliwa na Muungano wa Vyama vya CUF na CHADEMA Marekani.
Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV, walioka meza kuu wakanza kushoto Katibu wa Tawi la Chadema DMV Liberatus "Libe" Mwangombe, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tawi la Chadema DMV Mhe. Kalley Pandukizi, Shamis Alkhatry CUF pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la kina mama CHADEMA DMV Bi Baybe Mgaza. 

Kabla ya mkutano kuanza, picha ya juu na chini zinazofuata, zikionyesha  kisimamo cha dakika moja kumuombe na kada  na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM, John Komba

MC katika mkutano huo, Bw.Libe Mwang'ombe, aliyeumudu kuuendesha mkutano kwa utaratibu uliotakiwa na kwa usalama hadi mwisho bila jazba hadi mwisho masuali yaliulizwa kwa vifungu na kujibiwa ipasavyo  
 Dada Salma akiuliza suali kwa wakati wake, masuali mengi yaliulizwa na wadau mbali mbali ambyo yalikuwa ya msingi kwa mustakabali wa taifa letu
 Wajumbe waandalizi kutoka UKAWA wakiwa na mgeni wao Mh. Ismail Jussa kwa pamoja wakibadilishana mawazo

No comments: