ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 14, 2015

NGUMI KUPIGWA JUMAPILI UWANJA WA NDANI WA TAIFA MABONDIA WAZIDUNDA KAVU KAVU

Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakikunjana baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili katika uwanja wa ndani wa taifa 
Mabondia Mada Maugo kushoto na Kalama Nyilawila wakikunjana baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili katika uwanja wa ndani wa taifa 
Bondia Thomas Mashali akipima uzito
Bondia Japhert Kaseba akipima uzito kulia ni mpinzani wakeSaid Mbelwa akishudia kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa 
Bondia Said Mbelwa akipima uzito kulia ni mpinzani wake Japhert Kaseba akishudia kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa 
Mabondia Said Mbelwa na Japhert Kaseba wakitunishiana misuli baada ya kupima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa jumapili ya march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa 
Bondia Abdallah Pazi Akipima uzito

Na Mwandishi Wetu

MABONDIA Mada Maugo na Kalama Nyilawila nusula wazipige kavu kavu wakati wa upimaji wa uzito kwa ajili ya mpambano wao wa kesho jumapili mpambano utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa wakati wa upimaji uzito

Maugo alienda kumtambia Kalama na kumpiga kibao pamoja na teke kali sana lililompiga Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' wakati akiamulizia ugomvi uho hapo ndipo lilipozuka songombingo kali kwa mashabiki wa kambi zote mbili wakitaka kuzipiga kavu kavu uku maugo akiwa ameshapanda moli wa kupigana nje ya uringo

mpambano uho ambao utakuwa na michezo mingine ya kumaliza ubishi ni kati ya Thomas Mashali atakaemkabili Abdallah Pazi na Japhert Kaseba atapambana na Saidi Mbelwa mipambano hiyo yote yatafanyika siku ya jumapili march 15 katika uwanja wa ndani wa taifa

ambapo baadhi ya mashabiki wameomba baadhi ya daladala zinazofanya kazi usiku kwenda kuwa chukuwa pindi wamalizapo kuangalia mapambano hayo yaliyo na ushindani wa kweli


siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali

na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.

No comments: