Mabaki ya ndege ya ujerumani ilioanguka na kuwaua 150
Chumba cha rubani wa ndege
Hayo ni baada ya kufanya msako katika nyumba yake.
Polisi hawajatoa taarifa zaidi kuhusiana na kile walichokipata, lakini baadhi ya vitu vyake vikiwemo Kompyuta, vimechukuliwa ili kuchunguzwa.
Huku uchunguzi huo ukiendelea, imebainika kuwa rubani huyo alitatiza kwa muda, mafunzo yake ya urubani mwaka 2008, kutokana na kutibiwa matatizo ya kiakili
Waziri wa maswala ya ndani nchini Ujerumani, Tomas de Maiziere, anasema kuwa, uchunguzi wa kiusalama dhidi ya rubani huyo, haujasema lolote huku, muajiri wake kampuni ya Lufthansa, ikisizitiza kuwa Lubitz alikuwa asilimia mia kuendesha ndege
BBC
No comments:
Post a Comment