Tuesday, March 24, 2015

RAIS JAKAYA KIKWETE AWAFARIJI WAKAZI WA BUGURUNI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO

Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua kazi ya kuondoa maji ya mafuriko kutoka katika nyumba za watu katika eneo la Buruguruni Mnyamani wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam leo wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na kuwafariji wananchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji mmoja wa wakazi wa Buguruni Mnyamani Bi.Halima Hamza ambaye nyumba yake imeathiriwa vibaya na maji ya mafuriko wakati Rais na Mkewe Mama Salma Kikwete na viongozi mbalimbali walipotembelea eneo hili kujionea athari za mafuriko na kuwafariji wananchi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia mtoto Irene ambaye nyumba yao imeathiriwa na mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Rais Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita katika mitaa mbalimbali ya Buguruni leo wakati wa zoezi la kuwafariji waathirika wa mafuriko huko Buguruni Mnyamani leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Said Mack Sadik akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete mfereji ulioziba kutokana na uchafu na kusababisha mafuriko katika makazi ya watu eneo la Buguruni Mnyamani jijini Dar es Salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Buguruni Mnyamani waloathiriwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam.Rais Kikwete ameahidi kuwasaidia wananchi hao.

5 comments:

Anonymous said...

kazi kweli kweli hawa viongozi wetu wa Africa,hili tatizo siyo mara kwanza kutokea tena limeongezeka maradufu kutokana na utupaji holela wa taka na nyumba kujengwa kiholela,ni aibu kuona kiongozi wa nchi na kiongozi wa mkoa kufanya hizi ziara kila mara linapotokea wakati kuna ufumbuzi wake kama wakiwa serious,na wala haliitaji degree kulitatua,bonde la jangwani kuanzia vingunguti,tabata,jangwani klabu ya yanga ndiyo dampo la uchafu wote mpaka zile taka ngumu,cha muhimu kuwe na sheria kali ya kupiga marufuku utupaji ovyo wa taka,na matumizi ya mifuko ya plastiki yapigwe marufuku sababu ni chanzo cha kuziba mifereji mingi Tanzania na mbaya Zaidi hiyi mifuko ya plasiki haiozi,mbona Rwanda imepigwa marufuku na imesaidia kuweka mazingira safi,kwani sisI tunashindwa vitu ambavyo vipo ndani uwezo wetu?swali ni kwamba mafuriko yakitokea mwakani wataenda kuwapa pole tena hao wananchi au wata tafakari njia ya kumaliza tatizo hili? tuombe mungu,kazi kujisifu na VIKWANGUA ANGA.

Anonymous said...

Alafu watu wakiambiwa bongo tambarare wanabisha,nyie endeleeni kushangaa barabara huko ulaya wakati sisi tunapiga atua mbele hapa bongo,ni maendeleo kwa kwenda mbele bongo tumepiga atua sana.

Anonymous said...

mwakani itakua same story!!!...nothing new here.

Anonymous said...

Kikwete ni mafuriko au fashion show

Anonymous said...

Wenzetu wa nchi za majuu likitokea tatizo linakuwa kwao ni darasa. Lazima lifanyiwe utafiti na watahakikisha kuwa halijirudii. Hata likirudia haliwezi kuleta tena madhara kwa watu. Hapo kwetu Tanzania ni kichefuchefu tu kila mwaka shida ni ile ile. Tusitafute mchawi. Shida uongozi mbovu!!! Serikali itoe tu matamko ya KUPIGA raia wasiokuwa na hatia. Fungueni macho watanzania.