Advertisements

Wednesday, March 4, 2015

UKIWA NA MKE KAMA HUYU MUME NYUMBANI MAPEMA NA JIKONI ATAINGIA

Naomi Peter akitoa kipondo kwa mumewe.
UPEPO umegeuka! Imani ya kwamba wanaume ndiyo wamekuwa wakiwapa kipondo wake zao imegeuka, safari hii mwanamke aliyejulikana kwa jina la Naomi Peter akimpa kipondo ‘hevi’ mumewe John Shila mchana kweupe!
Wawili hao wakazi wa Misheni, jijini Mwanza waliibua timbwili la aina yake ambalo liliwavuta watu wengi chanzo kikiwa ni mwanaume huyo kumkataa mtoto aliyezaa na mwanamke huyo.

Akizungumza na waandishi wetu, mmoja wa mashuhuda alisema wawili hao walioana na kuishi kama mke na mume na baadaye kupata mtoto mmoja wa kike, baada ya miaka miwili ulitokea ugomvi na kusababisha mwanamke kuondoka na ndipo John alipotumia mwanya huo kuoa mwanamke mwingine.
Majirani wakiamulizia.

“Siku ya tukio, Naomi alimpeleka mtoto wake nyumbani kwa mzazi mwenzake kutokana na kutopewa hela ya matumizi, wakati huo Shila alikuwa na mwanamke wake mpya ndani, baada ya mabishano ya muda ndipo Naomi akaanza kumshughulikia Shila kwa kumtandika mangumi.

“Jamaa alikuwa hapeleki matumizi kwa mzazi mwenzie, mbaya zaidi alikataa na kudai mtoto si wake ndipo timbwili lilipoanzia,’’ kilisema chanzo hicho.

.
Atimaye kipondo kikiendelea.

Chanzo hicho kilizidi kueleza kuwa, wakati ugomvi huo ukiendelea mwanamke wa John wa sasa alikuwa kimya ndani na kushuhudia mpenzi wake akipokea kichapo kisha kumkabidhi mwanaye amlee na yeye akaondoka zake.

Hadi shuhuda wa habari hizi anaondoka eneo la tukio, muafaka juu ya kilichofikiwa ulikuwa bado haujapatikana.
\CREDIT:GPL

3 comments:

Anonymous said...

Hii nafikiri ,ni afadhali ,kumpiga mwanaume,ukimpiga ,mwanaume anakuheshimu,ukimuachia anakuwa malaya,kila miezi sita wanabadilisha ,wanawake.mimi kama mwanamke nakubaliana,wanaume waanze kupigwa ,inasaidia,

Anonymous said...

Sioni cha ajabu hapo mbona wanawake wanapigwaga? Basi na wanaume wapigwe pia

Anonymous said...

imenifurahisha habari hii kupita maelezo niko kibaruani na nimechoka na kazi mume ananizingua nikirudi nyumbani na pika na safisha mimi mshahara wangu anachukua kwenda kuleweya nabaki mnyonge tu sasa nilivyoona kuna mwanamke mwenzangu ana kwida mwanaume hivi imenifariji kweli natamani ningekuwa na nguvu kama zake na mimi nimkwide mume wangu.