NAIROBI, Kenya, March 6, 2015/ -- Ujumbe wa mawaziri na viongozi wakuu kutoka nchi za Afrika Mashariki wameahidi kuunga mkono harakati za kutafutia umwafaka tatizo la upungufu wa nishati.
Wazungumzaji muhimu kutoka Benki ya Dunia, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), IFC, Barclays, Symbion Power, KenGen, KPLC, UMEME na EEP watahutubu kuhusu hatua zinazoweza kuleta mabadiliko katika sekta ya nishati ikiwa ni pamoja na; nafasi muhimu ya usambazaji umeme katika mchakato wa kuendeleza viwanda, umuhimu wa nishati, jinsi ya kukabiliana na vizuizi vya mikopo na jinsi gharama ya mikopo katika kanda inaweza kupunguzwa kwa kuimarisha usambazaji umeme.
Meneja wa Mpango wa EnergyNet Bi. Ms Veronica Bolton-Smith alizungumza kuhusu hatua ya Mawaziri kukubali mialiko; “Ukizingatia kwamba mkutano huu unalenga washirika wachache, uwepo wa vigogo wanne katika sekta ya kibinafsi ya nishati katika kanda hii ni ishara ya haja ya kuwa na mdahalo wenye lengo.”
Ili kuona orodha kamili ya watakaotoa hutuba na ratiba kamili ya kikao hiki, tafadhali tembeleawww.powering-eastafrica.com, au jiunge na mjadala kwenye Twitter @EnergyNet_Ltd #poweringeastafrica
Distributed by APO (African Press Organization) on behalf of EnergyNet Ltd.
Kwa maelezo zaaidi jinsi ya kuhudhuria mkutano huu:
Tarehe: 25-27 Machi 2015
Eneo la Tukio: Windsor Golf Hotel & Country Club, Nairobi
Wasiliana na: Amy Offord, Meneja wa Masoko
Simu: +44 (0)20 7384 8068
Barua pepe: pe-a@energynet.co.uk
Tembelea: http://www.powering- eastafrica.com/
SOURCE
EnergyNet Ltd
No comments:
Post a Comment