Tuesday, March 10, 2015

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM WILAYA YA BAHI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi makubwa mara baada ya kuwasili katika wilaya ya Bahi.
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kujenga na kukiimarisha Chama mkoani Dodoma pamoja na kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilayni ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010.

 Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wananchi wa kijiji cha Nguji kabla ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kusalimia na kushiriki uchimbaji mitaro ya kutandikia ma bomba.

 Wananchi wa kijiji cha Nguji wakiwasikiliza viongozi wao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi wa kijiji cha Nguji na kuwataka watunze na kuilinda miundo mbinu ya maji iliyojengwa kijijini kwao.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (kushoto), Mkuu wa mkoa wa Dodoma Chiku Galawa wakishirikiana na wananchi wengine kuchimba mfereji wa kupitishia bomba la maji katika kijiji cha Nguji wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi makubwa katika kata ya Makanda kijiji cha Chonde wilaya ya Bahi mkoa wa Dodoma.
 Diwani wa kata ya Makanda Antony Boniface Liyamunda akisoma taarifa za miradi ya ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Chonde inayojengwa na nguvu za wananchi, pamoja na uzinduzi wa matrekta 19 yanayomilikiwa na vikundi vidogo vidogo kwa wakulima.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimia wananchi wa kijiji cha Chonde wilaya ya Bahi,mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chonde wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha trekta kama ishara ya kuzindua mradi wa matrekta 19 ya wakulima waliojiunga kwenye vikundi katiaka kata ya Makanda.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Chonde wilaya ya Bahi.
 Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma bango la wananchi wa kijiji cha Msisi ambao shule ya Msingi kwa Msisi iliondolewa paa na upepo mkali mwaka 2011 na haijaezekwa mpaka sasa mwaka 2015.
 Madarasa ya shule ya msingi Msisi ambayo yaliezuliwa paa na upepo mkali mwaka 2011
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kijiji cha Msisi ambao shule yao imeezuliwa paa tangia mwaka 2011.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiondoka katika eneo la shule ya msingi Msisi baada ya kukamilisha zoezi la kuichangia shule hiyo na itaanza kurekebishwa baada ya wiki mbili.
 PICHA ZAIDI

No comments: