Friday, March 13, 2015

ZIARA YA KINANA NA NAPE JIMBO LA MONDULI YAFANA

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasha umeme kama ishara ya kuzindua umeme katika kijiji cha Lolkisale.
Mradi wa umeme vijijini (REA) ni mradi unaodhaminiwa na serikali ya Tanzania kwa asilimia 100%.
Mbunge wa Jimbo la Monduli ,Waziri Mkuu Mstaafu Ndgu Edward Lowassa akiwasalimu wananchi wa Lolkisale mara baada ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuzindua rasmi umeme kijijini hapo.
Wananchi wa Lolkisale wakisikiliza hotuba za viongozi wao.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Lolkisale ambapo aliwapngeza kwa kuipa kura CCM kwenye chaguzi za serikali za mitaa.
Wananchi wa Lolkisale wakipiga makofi kushangilia hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi jengo jipya la hospitali ya wilaya ya Monduli kwa kushirikiana Mbunge wa Monduli, Waziri Mkuu mstaafu Ndugu Edward Lowassa.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupanga mawe kwa ajili ya sakafu wakati alipotembelea kijionea maendeleo ya jengo la kisasa la hospitli ya Monduli.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimia Viongozi na wananchi wa Monduli mara baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya majengo mapya ya hospitali ya wilaya ya Monduli.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Monduli mjini.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu wakazi wa Monduli mjini
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki palizi kwenye shamba la mpunga Mto wa Mbu,Monduli mkoani Arusha.
Vijana wa Mto wa Mbu wakishangilia CCM Oyee
Mbunge wa Viti Maalum Ndugu Namelok Sokoine akiwasalimu wananchi wa Mto wa Mbu na kuwaambia ni muhimu sana kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na kuwasihi kujitokeza kwa wingi mara tu baada ya tarehe ya kujiandikishwa kutangazwa.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Waziri kuu mstaafu Edward Lowassa kwenye viwanja vya mkutano Mto wa Mbu ,Monduli Arusha.
Wananchi wa Mto wa Mbu Arusha wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara ya kuzunguka nchi nzima ya kuimarisha na kukagua utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010.

No comments: