ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 27, 2015

BALOZI LIBERATA MULAMULA AIPONGEZA NA KUIMWAGIA SIFA ZANZIBAR HEROES

Balozi wa Tanzania nchini Marekani na Mexico amewapongeza wachezaji na viongozi wa Zanzibar Heroes kwa kunyakua kombe la Muungano kwa mechi iliyofanyika siku ya Jumamosi April 25, 2015 Capitol Heights, Maryland nchini Marekani.

Katika salamu za pongezi Mhe. Liberata Mulamula pia aliwashukuru Peoples Bank of Zanzibar kwa udhamini wao na kuwaomba kuendelea kuwa na moyo huo huo wa kuitambua Diaspora ni sehemu ya Tanzania na mchango mkubwa katika kusukuma gurudumu la maendeleo Tanzania.

Pia Mhe. Balozi Liberata Mulamula amewashukuru Viongozi na Wanajumuiya kwa kufanikisha sana sherehe hiyo iliyopekelea Rais mstaafu na ujumbe wake kufurahi kwa makaribisho mazuri waliyopata.

Mechi hiyo ilikua mechi ya pili ya sherehe hiyo ya Muungano katika mechi ya kwanza iliyochezwa mwaka jana na timu zote kutoka sare ya magoli na baadae kupigiana penati ambazo hazikumalizika kwa wachezaji kuwa na jazba kutokana na kukamiana sana kulikopelekea Ubalozi kuamua kukabidhi kombe kwa manahodha wa timu zote.

Mechi ya Jumamosi haikuonekana kama ni mechi ya timu ya Tanzania bara kufungwa  goli zote hizo 7-1 kutokana na mechi ya mwaka jana ilivyokua ambayo Zanzibar Heroes haikua na makali kama ilivyoonsha kwenye mechi hii iliyochezewa Capitol Heights pamoja na hali ya hewa kua ya baridi kiasi laikini mashabiki wa pande zote mbili waliangalia mpira mpaka mwisho.
Dedi Luba nahodha wa Zanzibar akikabidhiwa kombe na Bwn. Abdallah Makame amabye ni Katibu Mkuu wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi.
 Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV bwn. Idd Sandaly akiongozana na Mhe. Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi alipowasili uwanjani kusalimia na kukagua timu za mpira wa miguu kati ya Tanzania Bara na Zanzibar Heroes
Kwa picha za wachezaji wakisalimia na na Rais mstaafu bofya soma zaidi


4 comments:

Anonymous said...

Jamani Mzee Mwinyi yeye hakusema chochote ama yeye mmemzarau?

Anonymous said...

Hivi mbona MNA akili finyo hivyo, sababu hakikuandikwa hapa basi amedharauliwa? Grow up please you are very very narrow minded.
Learn to put things into perspective and read the heading of the post. And stay informed if you really care you should have seen that on previous posts.
By the way are you paying for this service? Get a clue people are working very hard to provide this information appreciate for a change.

Anonymous said...

I surely don't think the second observer here above responded to the query that was posed. Argue don't shout!! Insults do not add to a response.

Anonymous said...

Huyo anayetukana hata haeleweki. Naona ukweli umemkera kiasi cha kuchanganyikiwa