Advertisements

Sunday, April 19, 2015

KINANA ASHIRIKI BONANZA LA KUHAMASISHA WANANCHI KUJIANDIKISHA KWENYE DAFTARI LA KUPIGA KURA


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Viongozi na waratibu wa Bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika Daftari Maalum la kupiga kura mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Gonga, Karakata tayari kushiriki mchaka mchaka na vijana zaidi ya 500 kutoka vikundi mbali mbali vya wilaya ya Ilala na Temeke.


Vijana wakiwa wamekusanyika tayari kuanza kushiriki mazoezi ya jogging kwenye uwanja wa Gonga, Karakata ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.


Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana, Katikabu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (katikati) na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhan Madabida (kulia) wakisubiri utaratibu wa kuanza mazoezi ya mchaka mchaka (jogging) na vijana zaidi ya 500 ambapo mazoezi hayo yalibeba ujumbe wa kuhamasisha watu kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura.


Kikundi mwenyeji Kaza Roho ambacho kimeandaa Bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura wakijiandaa kuongoza mchaka mchaka (jogging)ambapo ilianzia Karakata,Jet na kumalizikia kwenye viwanja vya Social, Sitaki Shari.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye fulana ya rangi ya blu bahari) akikatiza mitaa ya Karakata wakati wa kushiriki jogging iliyoandaliwa na Kikundi cha Kaza Roho.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana (mwenye fulana ya rangi ya blu bahari)akishiriki mazoezi ya jogging pamoaja na viongozi wengine wa chama na serikali yalioandaliwa na kikundi cha jogging cha KazaRoho kutoka Sitaki Shari.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (mwenye kofia nyeusi) akishiriki kikamilifu kukimbia mchaka mchaka na vijana zaidi ya 500 kutoka wilaya ya Ilala na Temeke.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Segerea Ndugu Makongoro Mahanga wakati wa kupokea vikundi vya vijana kwenye viwanja vya Social ,Sitaki Shari .


Vijana wa Mnyama Jogging wakiingia kwenye uwanja wa Social, Sitaki Shari.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea bendera ya Taifa kutoka kwa kiongozi wa kikundi cha jogging Kaza Roho kama ishara ya kupokea vijana wa jogging kwenye viwanja vya Social Sitaki Shari jijini Dar Es salaam.


Viongozi wa Vikundi mbali mbali vya Jogging wakiongoza mazoezi katika viwanja vya Social, Sitaki Shari jijini Dar es Salaam.


Vijana wakishiriki mazoezi ya Pamoja.


Viongozi wa Vikundi vya Jogging pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiongoza vijana kufanya mazoezi.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki pamoja na vijana kufanya mazoezi ya pamoja kwenye viwanja vya Social Sitaki Shari.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiruka kutoka jukwaani kuonyesha ukakamavu wakati wa mazoezi ya pamoja na vikundi zaidi ya 30 vya jogging kwenye uwanja wa Social Sitaki Shari jijini Dar es Salaam.


Msaga Sumu akitumbuiza vijana wa mazoezi ya Jogging kwenye uwanja wa Social,Sitaki Shari.


Msanii wa siku nyingi ambaye alishawahi kuwa na kundi la Free Dogs Camp lililojuisha wasanii kama P wa Black, Nale Nale, OMG akitumbuiza kwenye bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwenye viwanja vya Social ,Sitaki Shari.


Wawakilishi wa Kikundi cha Kaza Roho Bi,Sabrina Yasin(kulia) na Herieth Noel wakisoma risala ya kikundi chao kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye viwanja vya Social, Sitaki Shari jijini Dar es salaam.


Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimu vijana kwenye uwanja wa Social ambao walihudhuria bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftrai la kudumu la kupiga kura.


Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na vijana wa jogging walishiriki bonanza maalum la kuhimiza wananchi wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la kupiga kura kwenye viwanja vya Social,Sitaki Shari jijini Dar es salaam.


Wasanii wa Yamoto Band wakionyesha umahiri wao kwenye Bonanza maalum la kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.

No comments: