Advertisements

Sunday, April 19, 2015

MADAMOTTO PRESS RELEASE

NA MWANDISHI WETU
KUTOKANA na kukithiri kwa ajali za barabarani nchini zilizosababisha vivyo vya takriban watu 1,000 waandaaji wa kipindi cha Mada Motto kinachorushwa katika kituo cha Channel Ten, wameamua kuandaa kipindi maalumu leo kitakachotafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

Akizungumza katika taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, mwandaaji wa kipindi hicho ambacho zamani kiliitwa Kitimoto, Ally Oki alisema walikuwa na mada nyingine kwa Jumatatu lakini wameamua kuiweka pembeni ili kuleta kipindi hicho maalumu.



Aidha, katika kipindi hicho watahusishwa madereva na wadau wa usafiri ili kujua chanzo cha ajali hizo ni nini hasa ikizingatiwa sekta ya usafirishaji inachangia asilimia kubwa ya pato la taifa.
“Ndugu zetu wengi wanapoteza maisha barabarani, wengine wanajawa na hofu hata kuahirisha safari zao kutokana na taarifa za ajali kila siku. Kuna tatizo linalohitaji ufumbuzi wa kudumu, tunaweza kuanza kwa kuwasikiliza madereva wana nini.

“Huwezi kujua inawezekana wana mambo mengi vichwani mwao hawana pa kusemea, lakini watu wa serikali tutakuwa nao na watakaoshindwa kuja wataungana nasi kwa njia ya simu, lakini majibu lazima yapatikane,” alisema Ally Oki.

Aliongeza kuwa katika kipindi icho kinachorushwa mara tatu kwa wiki kuanzia saa nne mpaka saa tano kwa leo kitarushwa kwa saa moja na nusu kutokana na umuhimu wake.

“Tangu tuanze kipindi wiki iliyopita tumekuwa tukitumia muda wa saa moja, kwa siku za Jumatatu, Jumatano na Ijumaa lakini kutokana na umuhimu wa suala hili la ajali tumeongeza nusu saa ili watu wapate muda mwingi wa kueleza mawazo yao,” alisema.

Alisisitiza kuwa kwa wale watakaokuwa mbali na luninga wanaweza kuchangia wanweza kutoa mawazo yao kwa njia ya mtandao wa kijamii facebook na tittwer aau tovuti ambazo ni (madamottotvshow/facebook , @madamottotvshow/twitter nawww.madamottotvshow.com).
Mpaka sasa kipindi hicho kimesharusha mada nne ambazo ni ajali za barabarani, mswada wa makosa ya mtandaoni (Cyber Crime), kwanini Tanzania masikini na namna gani tunakabiliana na maafa.

No comments: