Luol Deng Chris Paul
Chama cha Mpira wa Kikapu cha Marekani, NBA kimetangaza Jumatano mipango ya kucheza mchezo wake wa kwanza barani Afrika, katika mchezo wa mwezi Agosti ambao utawashirikisha wachezaji wa mpira wa kikapu barani Afrika katika jitihada za kuufanya mchezo huo kupata mashabiki duniani.
Mechi ya Agosti Mosi mjini Johannesburg itaundwa na timu ya Afrika "Team Africa" ikiwashirikisha wachezaji nyota wa mpira wa kikapu wa ligi ya NBA wa kizazi cha kwanza na cha pili kutoka Afrika dhidi ya timu ya dunia"Team World,"ambayo itakuwa na wachezaji kutoka maneo mengine duniani.
Mchezaji nyota mara mbili wa NBA All-Star, Luol Deng wa timu ya Miami Heat, ambaye alizaliwa katika nchi ambayo kwa sasa ni Sudan Kusini, ataongoza timu ya Team Africa, wakati nyota mara nane wa NBA Chris Paul wa Los Angeles Clippers atakuwa nahodha wa timu ya Team World.
Tangazo hilo limetolewa wakati ligi ya Marekani imetangaza kalenda yake ya mwaka kwa michezo ya nje kwa mwaka 2015-2016. NBA tayari imetangaza michezo nchini Brazil, China na Mexico.
Muundo wa mchezo wa Afrika unatofautiana kwa kiasi kikubwa na mashindano mengine ya nje ya NBA, ambayo inahusisha timu mbili za NBA au mchezo wa kabla ya msimu.
Uwanja wa Johannesburg, Ellis Park Arena, wenye viti 6,300, unaonekana kuwa mdogo zaidi ya viwanja kama O2 mjini London na Ulker Sports Arena mjini Istanbul, Uturuki ambavyo vimewahi kuwa wenyeji wa michezo ya msimu wa 2014-15.
Sal LaRocca, rais wa shughuli za kibiashara duniani wa NBA, amesema ligi hiyo "bado iko katika hatua ya mwanzo kabisa" ya kuendeleza Afrika kuwa soko la mpira wa kikapu.
"Kila eneo tulimoanzisha biashara yetu, kwa namna moja au nyingine, tulianza na mchezo," LaRocca ameiambia AFP.
"Kwa hiyo hiki ni kigezo muhimu katika maendeleo yetu barani Afrika."
Mpira wa miguu ni mchezo unaopendwa zaidi barani Afrika, na raga una mashabiki wengi nchini Afrika Kusini.
NBA ina ofisi 12 katika masoko ya kimataifa. Kubwa kuliko yote ni China, ambako inaajiri kiasi cha watu 130 mjini Beijing, Shanghai, Hong Kong na Taiwan.
NBA ilifungua ofisi yake mjini Johannesburg mwaka 2010 na kwamba sasa ina wafanyakazi 11 ambao wanasimamia mipango yote barani Afrika.
BBC
No comments:
Post a Comment