Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (katikati) akiangalia mbidhaa za tv zilizokutwa katika mojawapo ya kontena zilizokuwepo katika Bandari ya Nchi Kavu ya TRH katika ziara ya wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kushoto) akisikiliza maelekezo kutoka kwa Kamishna Msaidizi wa Forodha wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bw. Tiagi Kabisi katika ziara ya wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam ambapo kontena mbili zilikamtwa ambapo moja ilikutwa na bidhaa za tv na nyingine biskuti huku nyingine mbili hazikuweza kupatikana mahali zilipofichwa.
Kontena mbili zenye bidhaa za Tv na Biskuti zilizokamatwa katika Bandari ya Nchi Kavu ya Tanzania Road Haulage (TRH) wakati wa ziara ya Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (katikati) akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha (kulia) Mhe.Dkt.Servacius Likwelile na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA Richard Kayombo(kushoto) wakati wa ziara ya wizara hiyo katika Bandari ya nchi Kavu ya Tanzania Road Haulage(TRH)jana jijini Dar es Salaam.
Kamishna Msaidizi wa Forodha wa Mamalaka ya Mapato Tanzania (TRA),Bw. Tiagi Kabisi kushoto akipata maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Tanzania Road Haulage (TRH) Bw. Ali Lilani katika ziara ilifanywa na Waziri wa Fedha jana jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (katikati) akiwasili katika Bandari ya Nchi Kavu ya TRH katika ziara ya wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam ambapo kontena mbili zilikamtwa ambapo moja ilikutwa na bidhaa za tv na nyingine biskuti huku nyingine mbili hazikuweza kupatikana mahali zilipofichwa.
Na Lorietha Laurence- Maelezo
Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya amesema kuwa serikali itawashughulikia wafanyabiashara wanaokwepa kulipa kodi kwa kuwachukulia hatua stahiki ikiwemo kunyang’anywa leseni ya biashara na kulipa faini.
Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kukagua bandari kavu ya kampuni ya THR ambapo ni mjumuisho wa ziara iliyoanza jana jioni kutembelea Bandari za nchi kavu. “Tumekamata jumla ya kontena nane ambazo katika taarifa za awali zilieleza kuwa zina bidhaa za gypsum powder na gysum plasta lakini tulipozifungua tumekutana na bidhaa tofauti na kile tulichoambiwa” alisema Mhe. Mkuya
No comments:
Post a Comment