Mhe. Charles Kitwanga ( Mb) Naibu Waziri, Nishati na Madini akizungumzia namna Tanzania inavyotekeleza Mkakati wa Nishati Endelevu kwa Wote (SE4All) wakati wa Mkutano wa siku Mbili wa Mawaziri wa Sekta ya Nishani, uliofanyika hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Wataalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini ambao wamefuatana na Naibu Waziri katika mkutano huu muhimu uliojadili kwa kina nafasi na umuhimu wa nishati endelevu kwa wote katika kusukuma mbele malengo ya maendeleo endelevu , ukuaji wa uchumi, maendeleo ya jamii na utunzaji wa mazingira.
Mhe. Kitwanga akiteta jambo na Mwakilishi wa Bank ya Maendeleo kwaajili ya Afrika AfDB muda mfupi mara baada ya Naibu Waziri kuzungumza , mkutano huu wa SE4All, pamoja na Mawaziri wa sekta husika umewashirikisha pia wadau mbalimbali wakiwamo wakuu wa vyombo vya fedha kama vile Bank ya Dunia, AfDB na wataalamu wengine wakiwamo pia wanamziki maarufu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wakichagiza na kuwekeza katika nishati endelevu.
Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava akiwasilisha Action Agenda of Tanzania kuhusu SE4All katika moja ya mikutano iliyofanyika hapa jijini New York.
Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava akiwa na wataalamu wake na wataalamu washauri wakibadilishana mawazo kuhusu Action Plan of Tanzania.
Na Mwandishi
Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania inaamini kwamba, utekelezaji wa mipango
na malengo ya mbalimbali
ya maendeleo hayataweza
kupatika au kufikiwa kwa haraka pasi na uwepo wa nishati endelevu na kwa
wote.
Ni kutokana na
kulitambua hilo, Tanzania
imejikita kikamilifu katika
kukuza uwezeshaji wa matumizi ya teknolojia za kisasa na mbinu za
kuongeza upatikanaji wa huduma
za kisasa za nishati ikiwa ni pamoja na kuongeza maradufu kiwango cha
uboreshaji na ufanisi wa nishati mbadala
ili kuchagiza maendeleo.
Hayo yameelezwa siku ya
Alhamisi na Naibu Waziri wa Nishati
na Madini, Mhe. Charles Kitwanga ( Mb),
wakati akizungumza katika siku ya pili
ya majadiliano ya mawaziri wanaohusika
na sekta ya nishati ambapo kila
waziri aliyehudhuria mkutano huo
alipata fura ya kuelezea na
kutoa ahadi ya namna inavyotekeleza
mkakati wa nishati endelevu wa wote
(SE4All).
Mhe. Kitwanga na ujumbe
wake unaowashirikisha wataalamu mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Madini akiwano Kaimu
Katibu Mkuu, Bw. Ngosi Mwihava wameshiriki kikamilifu katika mkutano huu ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa, Ban Ki Moon, ambapo tangu
ulipoanza mapema wiki hii,
washiriki wamekuwa wakijadili mada mbali mbali zinazohusiana na masuala
ya nishati, uwekezaji na mchango
wake katika eneo zima la utekelezaji wa
malengo ya maendeleo endelevu.
“ Tanzania inaamini kwamba hakuna
ajenda za maendeleo zinazoweza
kufikiwa kwa ukamilifu pasipo uwepo wa
nishati ya uhakika” akasema Naibu Waziri
Na kuongeza kuwa, mkakati wa
nishati endelevu kwa wote ni nyezo muhimu katika kurahisisha ukusanyaji na uwekezaji wa raslimali
inayohitajika ili kufika malengo ya kitaifa ya
nishati endelevu kwa wote kufikia mwaka 2034 kama inayoainishwa
katika mkakati huo.
Kwa mujibu wa Naibu
Waziri, Charles Kitwanga, Tanzania
ilipitisha mkakati wa SE4All mwaka 2012 na kufuatiwa na mchakato wa kufanya tathmini ili kubaini mapungufu ambayo yalipelekea
kutoa taarifa ya tathmini mwaka 2013.
Baada ya tathmini hiyo ilifuatia misaada kutoka
SE4All kwaajili ya Afrika iliyosaidia kuandaa rasimu ya Ripoti na nchi ( Country Action Agenda) kwa ufadhili wa Banki ya Maendeleo
ya Afrika, (AfDB) na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ( UNDP).
Kwa mujibu wa Mhe. Kitwanga, taarifa
hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa
udhibitisho mwezi Agosti, 2015.
Aidha maandalizi ya Mpango wa Uwezeshaji umeanza na utalenga katika kuangalia
mahitaji ya haraka ili kuwezesha mpango huo kuanza kutekelezwa.
No comments:
Post a Comment