MABONDIA KUPIMA UZITO IJUMAA STEND YA BAGAMOYO KWA AJILI YA MPAMBANO WA JUMAMOSI
Na Mwandishi Wetu
MABONDIA Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo na Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam watapima uzito siku ya ijumaa katika stendi kuu ya mabasi Bagamoyo na kupigana siku ya jumamosi ya mei 16 katika ukumbi wa che kwa che
uliopo Bagamoyo mjini ambapo mabondia hawo watamalizia ubishi wao wa nani zaidi kati ya bagamoyo na Chanika
mpambano uho utakaosimamiwa na chama cha ngumi za kulipwa P.S.T litakuwa la raundi sita na kg 61 ambapo kutakuwa na mapambano mengine ya utangulizi siku hiyo yatakayowakutanisha bondia
Rashidi Haruna atakumbana na Kaminja Ramadhani na Harid Hongo atakabiliana na Kishoki Mbishi mpambano mwingine ni Abdallah Samata atakaye zidunda na Maono Alli
mipambano hiyo inaletwa kwenu na Sharif Promotion wakati mgeni rasmi siku hiyo ni bondia kutoka morogoro Cosmas Cheka ambaye atakuja kuwapa nasaa mbalimbali mabondia na mashabiki wa mchezo wa masumbwi kuweza kusonga mbele kwa mchezo uho mjini Bagamoyo
kingilia katika mpambano uho ni Tsh, 8000 kwa V.I.P na kwaida ni sh. 5000
Katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na upatikanaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi kali pamoja na kutambua sheria zake zikiwa na mabondia wakali kama vile
Floyd Mayweathar vs Manny Paquaio 2015 , Saul 'canelo' alverez ,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
pia kuta kuwa na vifaa vya mchezo vitakaokuwa vikigawiwa na kocha Rajabu Mhamila 'Super D' kwa mabondia watakaofanya vizuri siku hiyo na vingine kuuzwa kwa galama nafuu na kocha huyo kwa ajili ya kuamasisha mchezo wa masumbwi nchini
No comments:
Post a Comment