Advertisements

Sunday, May 10, 2015

MELI YA MV MAENDELEO YATIA NANGA SALAMA BANDARI YA UNGUJA BAADA YA KUKWAMA KWA MUDA KISIWANI PEMBA

Meli ya Mv Maendeleo iyokuwa iliyokuwa inataka kwenda Unguja ikitokea Pemba  imekwama kwa muda wa masaa kadha katika eneo la bandari ya Mkoani Kisiwani Pemba kutokana na kukwama katika fungu la mchanga na kushindwa kuondoka.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, kufuatai tukio la meli ya Mv Maendeleo kukwama katika fungu la mchanga na kushindwa kuondoka asubuhi hadi jioni ndipo ilipofanya safari ya kwenda Unguja.
Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, watatu kutoka kushoto akiwa na Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka na viongozi wa bandari wakiangalia jinsi gani meli hiyo itavyo ondoka bandarini hapo.
Naibu katibu Mkuu UVCCM Taifa Zanzibar Shaka Hamdu Shaka, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali vya habari, juu ya Tukio la kukwama katika fungu Meli ya Mv Maendeleo na kushindwa kuondoka jana asubuhi na kuondoka Jioni yake, baada ya maji kujaa na kuruhusiwa kuondoka.
Gari la zimamoto likiwa tayari katika bandari ya Mkoani, kwa ajili ya kutoa huduma ya dharura wakati wowote litakapo hitajika, baada ya meli ya Mv Maendeleo kukwama na kushindwa kuondoka bandarini hapo hadi maji yalipojaa jioni huku ikiwa na abiria 263.
Wananchi  mbali mbali wakiangalia Meli ya Mv Maendeleo ikiondoka kisiwani Pemba, baada ya maji kujaa na kukwamuka na kuanza safari ya kuelekea Unguja jana jioni.
Naibu katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka, wakati akitoka katoka katika bandari ya mkoani Kisiwani Pemba, baada ya meli ya Mv Maendeleo kukwamuka na kuruhusiwa kuondoka Mkoani na kuelekea Unguja.(Picha na Abdi Suleiman, PEMBA.)

Meli ya Mv Maendeleo imetia nanga salama katika bandari ya Unguja ikitokea kisiwani Pemba baada ya kukwama kwa muda wa masaa kadha katika eneo la bandari ya Mkoani.


Akizungumza kwa njia ya simu kutoka bandarini Unguja na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazanzibari nchini Marekani (ZADIA) Bwana Omar Haji Ali, Afisa wa ngazi za juu katika MV Maendeleo alithibitsha kuwa meli hiyo imetia nanga ikiwa na abiria wote salama.


"Siwezi kuzungumza sana kwa sasa kwa vile bado tumo katika harakati za kushusha abiria", alisema afisa huyo na kuongeza kuwa atakuwa katika nafasi nzuri zaidi ya kuongea baadaya mkutano na maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Zanzibar utakaofanyika mara tu baada ya kumaliza ushushaji wa abiria hao.

Mawasiliano ya Ndugu Omar Ali na maofisa wa ngazi za juu katika Serikali ya Zanzibar na MV Maendeleo, yankuja katika juhudi za kuwapatia taarifa za uhakika wanachama wa ZADIA na Wazanzibari kwa ujumla nchini Marekani, kufutia khofu na mtafaruku vilivyojitokeza miongoni mwa wanajumuiya hiyo baada ya habari za kukwama kwa meli hiyo kisiwani Pemba.

Bwana Ali amewataka wanajumiya hiyo kutokuwa na khofu yoyote juu ya ndugu na jamaa zao waliokuwa katika meli hiyo, kwani abiria wote wamefika salama salmini.

Meli ya Mv Maendeleo ilikwama baada ya kukosea njia wakati ikitoka katika banndari ya Mkoani kisiwani Pemba ikiwa na abiria zaidi ya 260. 

Bado haijajulikana rasmi ni hasara gani za kiuchumi zilizosababishwa na mkwamo huo wa abiria ambao baadhi yao walikuwa katika safari za kibiashara.

Taarifa zaidi baada ya mazungumzo na maofisa wa ngazi za juu wa MV maendeleo. Kwa hisani ya ZanziNews

1 comment:

Anonymous said...

DJ Luke tuache ushabiki kwa kisiasa. Title ya habari ni MV Maendeleo naadae munaandika habari za kisiasa kwa nini usingaliandika habari tofauti