Mh mbowe alipata nafasi ya kuzungumza na viongozi wa madereva hao.Mh Mbowe alipotaka kuzungumza na madereva hao microfone zote zilizimwa na kufichwa kusikojulikana jambo ambalo lilifanya ashindwe kusikika kwa madereva hao na kuamua kumtoa nje na kusukuma gari yake hadi maeneo ya shekilango na kurudi ofisini.
Mgomo wa Madereva uliodumu kwa takriban siku moja na ushee, hatimaye umepata muafaka baada ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Paul Makonda (pichani) kufanikiwa kuusuluhisha kwa kusaini makubaliano na Uongozi wa Chama cha Madereva.
Makubaliano hayo yaliitaka Serikali kuboresha Mikataba kwa Madereva, malipo kwa madereva hao, pamoja na tatizo la ukaguzi wa magari ili kuondoa usumbufu kwa madereva hao, na kuiomba Serikali kufanya ukaguzi huo kwa siku moja tu.
Akizungumza na Madereva hao, Mhe, Makonda amewataka Madereva hao kuachana na mgomo huo na kuwaahidi Madereva hao kuyafanyika kazi madai yao katika muda ambao wamekubaliana usiozidi saa 4 asubuhi kesho.
Aidha, Mhe Makonda amesema katika madai hayo imeundwa Tume ambayo itashughulikia madai hayo pamoja na kuwahakikishia Madereva hao kuwepo na mwakilishi katika Tume hiyo iliyoundwa, ambayo itajadili masuala ya Mkataba, malipo, matibabu pamoja na suala la kusoma kwa Madereva hao.
Pia Makonda amelitaka Jeshi la Polisi kupitia Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni kuwaachia Madereva ambao tayari walikua wamekamatwa kutokana na kuonekana kufanya fujo katika mgomo huo katika Soko la Urafiki jijini Dar es Salaam.
Kwa Upande wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Madereva, Bw. Rashidi Salehe amemuomba Mkuu wa Wilaya kutatua madai ya Madereva hao ili kuondoa mgomo ambao unakwamisha usafirishaji wa abiria.
4 comments:
VIVA CHADEMA
Hongera sana Mh. Paul Makonda kwa kumfunika Mh. Samwel Sita, MUNGU akubariki sana. Sasa wewe ndio umekuwa Waziri wa Uchukuzi. Hivi Mh. Samwel Sita, kama jambo dogo tu la mgogoro wa madereva limekushinda, utawezaje kuongoza nchi? Kama Wizara moja tu ya Uchukuzi imekushinda, je utaweza Wizara zote? Hili linatufundisha sote Watanzania kuwa Rais ajaye apimwe kwa kazi alizozifanya, sio kwa umaarufu. Makonda anaonekana kufanya kazi nzuri kwa nafasi ndogo aliyonayo ya DC. Ukimpa Ukuu wa Mkoa yawezekana akafanya makubwa zaidi. Kwa mfano huu wa Makonda, mpaka sasa sijaona Rais atakayetufaa katika orodha ya wale wote waliotangaza na walioombwa kugombea Urais. Ndugu Watanzania tukitaka kwenda kwenye level nyingine ya maisha, tunahitaji sura ngingine kabisa tofauti na wale waliojitokeza. Tunahitaji watu ambao watatuonyesha wamewafanyia nini WaTZ kwa nafasi walizopewa.
Wadau hapo juu tafadhali achane utani. Madereva wa mabasi ni suala dogo sana katika masuala mengi muhimu ya nchi. In fact, hao madereva wanayo bahati kuwa bado kazini, maana wangekuwa katika nchi nyingine, wote wangepewa pink slips! Nakumbuka hapa Marekani enzi za Rais Reagan aliwatimua Air-traffic controllers wote ambao walioweka mgomo nchini. Nadhani bongo tunaweza kutoa fundisho kama hilo endapo kutatokea tena migomo ya kijinga kama hii.
KAZI NZURI LAZIMA TUITAMBUE WATANANIA.
WOTE WALIOFIKA KWENYE HUU MGOMO Mhes. MBOWE NA P. Makonda Tunawapongeza sana. Ila tu kitendo cha kumzimia Mhesh. MBOWE vipaza sauti nayo sio uungwana na haki kwa wanaodai maslahi yao. Tunatambua ni jinsi gani serikali iliyopo madarakani inawanyima haki wataka haki.
Post a Comment