Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania akihojiwa na Priscilla Lecomte wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Umoja wa Mataifa. (Picha: UN/JosephMsami)
Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa jopo la Umoja wa Mataifa la kusaka jinsi dunia inaweza kukabiliana na magonjwa ya mlipuko kwa siku za usoni, amesema leo kwamba anatarajia kutoa mapendekezo juu ya mapugunfu yaliyoonekana wakati wa kupambana na Ebola.
Akihojiwa na Priscilla Lecomte na Jospeh Msami wa idhaa hii, ameeleza kwamba wanachama wa jopo hilo baada ya kuzungumza na wataalam wa afya mjini new York, watatembelea Geneva, Uswisi, ili kujadiliana na wadau wa shirika la afya ulimwenguni, WHO na mashirika mengine, halikadhalika watasafiri kwenda nchi zilizoathirika na Ebola.
Hapa Rais Kikwete anaanza kwa kuelezea jukumu la jopo hilo ambalo ripoti yake ya awali wataiwasilisha mwezi Septemba, ripoti ya mwisho ikitarajiwa mwisho wa mwaka .
KUSIKILIZA BONYEZA HAPA
2 comments:
As usual..talk talk talk wakati Muhimbili hospital pale pale Dar es salaam haina hata maji ya kunawa mikono na vitanda ndiyo usiseme.Na huyu huyu JK amekuwa madarakani kwa miaka 10!!! sasa jiulize hizo hospitali za mikoani zikoje? Hivi EBOLA ikiingia TZ na kuanza kuua watu mtawalawaumu WAZUNGU kwa kushindwa KUTOA MISAADA HARAKA????????
CHARITY BEGAN AT HOME
Post a Comment