ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 15, 2015

MAONYESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA KUFUNGULIWA JUNI 16

TANGAZO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


OFISI YA RAIS – MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA



Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
inawakaribisha wananchi na wadau wote katika maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Tarehe 16-23 Juni, 2015

Mahali: Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam

Kaulimbiu: “Utumishi wa Umma katika Bara la Afrika ni Chachu ya Kuwawezesha Wanawake, Kuongeza Ubunifu na Kuboresha Utoaji Huduma kwa Umma”.

Ushauri  na Huduma mbalimbali zitatolewa na wataalamu kutoka katika  Taasisi za umma bila malipo.

Ufunguzi utafanywa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani (Mb), na siku ya kilele Tuzo zitatolewa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mh. Ali Hassan Mwinyi.

Tarehe 17 Juni, 2015 Kongamano la Wiki ya Utumishi wa Umma litafanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) na ufunguzi utaongozwa na  Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue, na Msemaji Mkuu atakua Katibu Mkuu Kiongozi mstaafu Balozi Dkt. Matern Lumbanga.

Hakuna kiingilio katika maadhimisho haya, wananchi wote mnakaribishwa.

Limetolewa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
K.n.y; KAIMU KATIBU MKUU (UTUMISHI).

No comments: