Mwigulu Nchemba na familia yake wakiwasili kwenye ukumbi kwa ajili ya kutangaza nia ya kuwania nafasi ya kugombea Urais kupitia CCM mkoani Dodoma.
Kauli mbiu ya Mwigulu ni ‘Mabadiliko ni Vitendo Wakati ni Sasa.’
Katika hotuba yake Mwigulu ameanza kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu, wazee, ndugu zake, wananchi wake wa Iramba na wananchi wote waliohudhuria hafla hiyo ya kutangaza nia.
Mwigulu pia amempongeza Rais Kikwete kwa kumuamini na kumteua katika nyadhifa mbalimbali.
Amesema ameamua kutangaza nia akiwa mkoani Dodoma ili kuondoa dhana ya ‘ukwetukwetu’ iliyozoeleka miongoni kwa viongozi. Aongeza kuwa Dodoma ni makao makuu ya taifa na chama chake ndiyo maana amefanya hivyo.
Aidha Mwigulu ameeleza mambo matatu yaliyomsukuma kutangaza nia kuwa ni pamoja na:
-Kutaka Mabadiliko
-Kujua mbinu za mabadiliko
-Utayari wa kufanya mabadiliko.
Pia kiongozi huyo amekemea viongozi wanaochaguliwa kwa mazoea wakisingizia uzoefu kwa kueleza kuwa kiongozi anayechaguliwa kwa mazoea ataongoza kwa mazoea na atafanya kazi kwa mazoea maana uzoefu ni mazoea.
Kiongozi huyo ameeleza jinsi anavyozijua fika shida za Watanzania na umasikini walionao hajausoma kwenye vitabu bali ameishi maisha ya umasikini.
Mwigulu ameeleza pia alivyobeba zege baada ya kumaliza chuo kikuu na mke wake akiwa mama ntilie akiwapikia yeye na vibarua wengine wa ujenzi.
GPL
2 comments:
Urais sasa kila mtu anaweza. siyo tena kitu cha kuogopwa kama mwanzo. Mungu ibariki Tanzania na watu wake
Kaka Mwigulu kila mtu alianzia mbali hadi hapo alipo leo....hakuna hata mmoja aliyekuja kujikuta anacho cheo au fedha, nadhani hata Kikwete au Lowassa walipokuwa na umri kama wako walihangaika hivyo kama ulivyo hangaika wakati ulivyomaliza university. Wote tumetoka kwenye umaskini wa kutupwa....kumbuka definition ya Development kama inavyosema kwenye DEVELOPMENT STUDIES' lakini yote tunasahau kwa sababu maisha yanaenda mbele....wote tulikuwa maskini wa kutupwa...wengine hatukuwa na mahali pa kulala.....lakini kwa jitihada tumejikwamua. Ushauri wangu---ukimuona mtu aliyefanikiwa sana huko kwenu mnamwita tajiri, hakuzaliwa hivyo bali amehangaikia maisha hadi alipofikia na ni bahati katika nchi zetu hakuna limit unapotaka kurekebisha maisha yako, hakuna wa kukuzuia.
Post a Comment